Wakulima wa korosho kulipwa pesa zao

Wakulima wa korosho kulipwa pesa zao

Kijana kijana

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2018
Posts
2,546
Reaction score
2,625
Habarini wakuu,majuzi nimebahatika kuongea na mama mzazi huko nyumbani ambae alikuwa kila akinipigia simu basi analalamika kuhusiana na suala la korosho.

Nimeshangaa akiongea kwa furaha mama yangu mzazi akisema "baba kumbe tuliingiziwa pesa zetu kwenye akaunti watu wameshtukia baada ya kwenda kuangalia salio,ila wapo wachache ambao hawakulipwa bado"

Baada ya hayo tukazungumza kumbe wengi wameshalipwa pesa zao waliobaki wengi wao ni wale ambao sio wakulima(chomachoma)wanaonunua korosho za wakulima wakati wa shida,japo wapo wengine hawakulipwaa na ni wakulima,ila ni 30% kati ya 100% ambao hawakulipwa.

Kumbe huko kusini bwana wananchi hawakujiunga na huduma ya NMB mobile ambayo inakuwezesha kupata ujumbe mpaka kwenye simu yako pale salio linapoingia,sasa kuna ambao walibahatisha kwenda tizama salio kumbe pesa tayari,walipowahoji watu wa bodi ya korosho wakasema "Akupe nani taarifa na pesa yenyewe(songola)hamna?"

Wakulima wengi wana furaha kubwa huko kusini na huku wachache ambao hawajalipwa wakiliwaziwa na wengi waliolipwa pesa za korosho.

Hata hivyo msimu wa mwaka jana ulikuwa ni wa neema kubwa sana kuliko mwaka wowote ule(ngoma ikivumaa)

Licha ya hayo watu wasitarajie kubadilika kwa misimamo ya kisiasa ya watu wa kusini kwa suala la korosho kwa sababu wengi wao wameemeka na pesa hizo ambazo zimetolewa na serikali.

JF inaongea sana wakati huo muongeaji yuko dar pale sinza anapoga bia,huku sisi wenyewe wana kusini tunawasiliana na ndugu wanatusimulia namna wanavyonunua bati kwa ajili ya kuimarisha nyumba zao kutokana na pesa za korosho.

Ninachowashauri kwamba suala la korosho watu wakilitumia kwa ajili ya kukiangusha chama flani huko kusini basi watafeli,watu(wakulima wengi) bado wanafurahika sana na maamuzi hayo ambayo yamewafaidhisha mama zetu na baba zetu.

Wakulima wanafurahi wakati huo walanguzi wananuna,nawapa pole walanguzi wawe na subra serikali ikiamua imeamua kwani nayo inaamuliwa na watu,lakini lengo kuu ni kuwanufaisha wakulima wa korosho na wamenufaika,huyo mlanguzi ajue tu kwamba biashara ni faida na hasara.

Mkulima wa korosho hapati hasara.
Nawatakia siku njema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inawezekana ikawa kweli!

Swali, kwa nini wasipewe taarifa kwa wale ambao hawana akaunti za kibenk kuweza kujua kama wameingiziwa pesa zao?

Haya mambo yapo kienyeji enyeji tatizo, au tunafanya kwa mazoea?

Sijui kulikuwa na ulazima gani wao kuingza pesa ktk akaunt za kibenk bila wahusika (wauzaji korosho) bila kujua.?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habarini wakuu,majuzi nimebahatika kuongea na mama mzazi huko nyumbani ambae alikuwa kila akinipigia simu basi analalamika kuhusiana na suala la korosho.

Nimeshangaa akiongea kwa furaha mama yangu mzazi akisema "baba kumbe tuliingiziwa pesa zetu kwenye akaunti watu wameshtukia baada ya kwenda kuangalia salio,ila wapo wachache ambao hawakulipwa bado"

Baada ya hayo tukazungumza kumbe wengi wameshalipwa pesa zao waliobaki wengi wao ni wale ambao sio wakulima(chomachoma)wanaonunua korosho za wakulima wakati wa shida,japo wapo wengine hawakulipwaa na ni wakulima,ila ni 30% kati ya 100% ambao hawakulipwa.

Kumbe huko kusini bwana wananchi hawakujiunga na huduma ya NMB mobile ambayo inakuwezesha kupata ujumbe mpaka kwenye simu yako pale salio linapoingia,sasa kuna ambao walibahatisha kwenda tizama salio kumbe pesa tayari,walipowahoji watu wa bodi ya korosho wakasema "Akupe nani taarifa na pesa yenyewe(songola)hamna?"

Wakulima wengi wana furaha kubwa huko kusini na huku wachache ambao hawajalipwa wakiliwaziwa na wengi waliolipwa pesa za korosho.

Hata hivyo msimu wa mwaka jana ulikuwa ni wa neema kubwa sana kuliko mwaka wowote ule(ngoma ikivumaa)

Licha ya hayo watu wasitarajie kubadilika kwa misimamo ya kisiasa ya watu wa kusini kwa suala la korosho kwa sababu wengi wao wameemeka na pesa hizo ambazo zimetolewa na serikali.

JF inaongea sana wakati huo muongeaji yuko dar pale sinza anapoga bia,huku sisi wenyewe wana kusini tunawasiliana na ndugu wanatusimulia namna wanavyonunua bati kwa ajili ya kuimarisha nyumba zao kutokana na pesa za korosho.

Ninachowashauri kwamba suala la korosho watu wakilitumia kwa ajili ya kukiangusha chama flani huko kusini basi watafeli,watu(wakulima wengi) bado wanafurahika sana na maamuzi hayo ambayo yamewafaidhisha mama zetu na baba zetu.

Wakulima wanafurahi wakati huo walanguzi wananuna,nawapa pole walanguzi wawe na subra serikali ikiamua imeamua kwani nayo inaamuliwa na watu,lakini lengo kuu ni kuwanufaisha wakulima wa korosho na wamenufaika,huyo mlanguzi ajue tu kwamba biashara ni faida na hasara.

Mkulima wa korosho hapati hasara.
Nawatakia siku njema

Sent using Jamii Forums mobile app
Afadhali useme wewe mwenyewe mkulima.
Mimi hivi karibuni nilikuwa huko na moja ya tatizo lililochelewesha malipo ni verification ambapo kuna wakati kuna jina la mtu mmoja linajitokeza kwa zaidi chama kimoja cha ushirika. Malipo kupitia benki pia yamechangia kwani wengi wao hata hizo account zao walikwisha zisahau [dormant] na mwisho ni hao akina kangomba ambao wamejitahidi kuingiza siasa kwenye kadhia hii.
Maoni yangu ni kwamba mambo yatakuwa mazuri zaidi mwakani.
 
We walioandamana Masasi hadi kwa mkuu wa wilaya ni wa kasakazini?... Acha kuungopea UMA
Nakuambia wengi wao wamelipwa,au unakataa kama wengi wao hawajalipwa?

Kusini kuna wilaya zaidi ya 12 we unasema wilaya ya masasi wameandamana,unaelewa nachoanduka mkuu?

Mimi ninachokisema ni kwamba wengi wao wamelipwa pesa zao kuliko ambao hawakulipwa.

Unabisha??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: UCD
Afadhali useme wewe mwenyewe mkulima.
Mimi hivi karibuni nilikuwa huko na moja ya tatizo lililochelewesha malipo ni verification ambapo kuna wakati kuna jina la mtu mmoja linajitokeza kwa zaidi chama kimoja cha ushirika. Malipo kupitia benki pia yamechangia kwani wengi wao hata hizo account zao walikwisha zisahau [dormant] na mwisho ni hao akina kangomba ambao wamejitahidi kuingiza siasa kwenye kadhia hii.
Maoni yangu ni kwamba mambo yatakuwa mazuri zaidi mwakani.
Hapa nimezungumza uhalisia kwamba wengi wamelipwa,wakiwemo walezi wangu miminashangaa humu jf watu wanazidi kutoa nyuzi kukicha kana kwamba IDADI KUBWA HAWAJALIPWA KUMBE WACHACHE NDIO AMBAO HAWAJALIPWA NA KATIKA HAO WACHACHE KUNA HAO CHOMACHOMA WAMO HUMO HUMO.

Sikatai kwamba wapo wakulima halali ambao hawajalipwa,lakini watu wanafanya kama hakuna alolipwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi, ikiwa wakulima 100 waliuza korosho zao, halafu mkawalipa 70 kati yao. Na labda wakalipwa wale wenye kuwadai kiduchu tu, Je matasema wakulima woooote weshalipwa?? Tumia lugha nyingine hii; Mhhh.
Kwani amesema wote wamelipwa??
 
Hivi, ikiwa wakulima 100 waliuza korosho zao, halafu mkawalipa 70 kati yao. Na labda wakalipwa wale wenye kuwadai kiduchu tu, Je matasema wakulima woooote weshalipwa?? Tumia lugha nyingine hii; Mhhh.
70% ?????? statistically hii ikoje?
 
Ni kweli Wameanza kuwalipa ingawa ni wale wenye kilo chini ya tani 2............... na hawa ndio wenye uhitaji wa haraka na Pesa................
Yes mkuu,wengi wenye zaidi ya tani 2 wanunuzi wa chomachoma ambao wananunua kutoka kwa wakulima,lakini nao wana haki ya kupata.

Amgalia mimi mzee wangu kwa mwaka analima gunia kama 17 mpaka 20 za korosho,huku anahitajia zaidi ya mwenye tani 2.mwenye tani 2 hawezi kufa njaa kama mzee wangu mimi.

Na hao watalipwa wakikidhi vigezo vya serikali walivyoviainisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakuambia wengi wao wamelipwa,au unakataa kama wengi wao hawajalipwa?

Kusini kuna wilaya zaidi ya 12 we unasema wilaya ya masasi wameandamana,unaelewa nachoanduka mkuu?

Mimi ninachokisema ni kwamba wengi wao wamelipwa pesa zao kuliko ambao hawakulipwa.

Unabisha??

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha porojo.. we sema MAMA YAKO MZAZI NDO KALIPWA...
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom