Wakulima CHAURU wafisadiwa na viongozi wao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakulima CHAURU wafisadiwa na viongozi wao

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rosena, Sep 13, 2012.

 1. R

  Rosena Member

  #1
  Sep 13, 2012
  Joined: Sep 11, 2012
  Messages: 51
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jamani chama cha wakulima wa mpunga Ruvu CHAURU wamefanyiwa vitendo vya kifisadi na viongozi wao baada ya kulipia mashamba kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji na wengine kujikuta wakikosa kugawiwa mashamba hayo waliyoyalipia na wengine waliofanikiwa kulima mashamba hayo wamekosa huduma ya maji na kujikuta wakipata hasara kubwa sana. Pamoja na hasara hiyo kwa wakulima hao, viongozi wa CHAURU hawajatoa maelezo yoyote kana kwamba hakuna baya lililotokea.

  Kiukweli wanaCHAURU wanahitaji msaada mkubwa toka wizara ya kilimo ikiwa ni pamoja na kuletewa wataalam wa kilimo kwani pale kuna wababaishaji tu na waganga njaa. Hatuwataki viongozi walio madarakani wajiuzuru.Tumeitikia mbiu ya kilimo kwanza kwa bidii lakini jamaa hasa mwenyekiti wamekula pesa yetu bila aibu.

  Waziri wa kilimo tunaomba msaada wako tafadhali. Viongozi CHAURU wanatoa rushwa za kuwalimia bure wakubwa ili wasiulizwe kinachoendelea. Pia vigogo wa ushirika mkoa na wilaya wanakula nao ili kuficha uozo huu na kula fedha za ruzuku.
  Nawasilisha kwa uchungu sana.
   
Loading...