tutafikatu
JF-Expert Member
- Dec 17, 2011
- 3,307
- 4,585
Kuna hii taasisi inaitwa Equity for Tanzania (EFTA) inayodai inakopesha vifaa vya ujenzi imenipa utata.
Dada yangu ni mjasiriliamali wa kutengeneza matofali, nyanda za juu kusini. Hivi karibuni alinishirikisha kwamba anataka kuchukua mkopo wa milioni 30 wa vifaa vya ujenzi kwa hao EFTA tawi la Mbeya, ambapo wanashirikiana na Equity Bank Mbeya mjini. Kitu ambacho kimetushangaza ni kwamba hiyo ofisi inayodaiwa ni ya EFTA Mbeya mjini wanataka 20% ya milioni 30 ilipwe ofisini cash (ati ni pesa ya ofisi) kabla ya mkopo kuwa processed. Cha ajabu ni kwamba hata hizo mashine hawatengenezi wao, bali inabidi uwasiliane na mtengenezaji, ambaye inabidi akupe invoice, ambayo ndiyo itapelekwa benki.
Huhitaji kuwa na akili kubwa sana kujua kuwa huu ni uhuni, lakini najiuliza kama huu uhuni ni wa wafanyakazi wa EFTA tawi la Mbeya au EFTA kwa ujumla?
Inabidi tujuzane ili watu wasije wakalizwa...