Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Raia kutoka DR Congo ambao walikuwa wanasoma pamoja na mjapan mmoja kwenye chuo kimoja kule Ukraine miaka kadhaa iliyopita, walikuwa na tabia ya kuongea mambo mabaya tu kuhusiana na nchi yao.
Yule mjapan akawa kila akiingia kwenye chumba cha hostel cha hao wanafunzi wawili kutoka DR Congo, anasikia malalamiko tu, jinsi ambavyo kila wanachokiongelea kuhusiana na siasa za nchi yao, kilivyokuwa kimejaa laana badala ya baraka.
Siku moja mjapan akawaambia katika lugha kama ya utani vile, mnaonaje tubadilishane nchi, nyinyi watu wote wa DR Congo mpande ndege halafu muende kwetu Japan. Halafu sisi wajapan wote tupande ndege twende kwenu DR Congo. Baada ya miaka mitano mje DR Congo kuiona nchi yenu halafu na sisi tuende Japan kuona maendeleo mtakayokuwa mmeshayafanya kwenye nchi yetu.
Wale jamaa kutoka DR Congo wakabaki wakitazamana na kujiona ni kwa jinsi gani ambavyo kupitia maongezi yao, wanaidharaulisha nchi yao na mwisho wa siku hata wao pia wanageuka kuwa vituko mbele ya watu wa mataifa mengine.
Mjapan yule kwa kuona kuwa ujumbe wake umeeleweka, akaongeza dozi kwa kuwaambia wale jamaa kutoka DR Congo kwamba wao wajapan watachukua nguo tu, kwa ajili ya safari ya kwenda nchi ya mbali, kwani kile walichonacho kichwani kinatosha katika kuijenga DR Congo ikawa ni nchi yenye kuheshimika duniani.
Watanzania tuna tabia kama za hao wakongomani ambao mjapan alikuwa akiwashangaa jinsi wanavyoizungumzia kwa dhihaka nchi waliyozaliwa ingawa ina kila aina ya fursa ambazo mjapan anaamini kwamba wajapan wenzake watahitaji mabegi ya nguo kutoka Tokyo na ndege kwenda kuanza maisha mapya Kinshasa au Lubumbashi.
Kwa akili zetu hizi zinazopenda manung'uniko yasiyo na mwisho, sio ajabu ukiwachukua wajerumani ukawapa hii nchi yetu halafu sisi watanzania wote tukaenda kuishi Ujerumani hii ya sasa, baada ya miaka mitano Tanzania ambayo itakuwa ni mali ya wajerumani, ikawa ni tajiri kuliko Ujerumani waliyokabidhiwa watanzania milioni 49.
Adui wa maendeleo ya Tanzania wakati mwingine ni mawazo mgando ya mtanzania mwenyewe. Adui wa maendeleo yetu ni fikra zinazoangalia kutofanikiwa kwetu, tena wakati mwingine hata kabla hatujaanza kufanya jambo fulani.