Wakili wa kujitegemea, Awadh A. Said Zanzibar atoa ufafanuzi wa kauli ya Prof Kabudi kuhusu mamlaka ya JMT kwa Zanzibar

Hivi una uhakika zikipigwa kura za eidha kuuvunja ama kuuacha, wabara watachagua kuuacha na wazenj watachagua kuuvunja? Usiwasemee wenzako, posibo wewe ni sehemu ndogo sana ya wazanzibar. Mambo ya kisheria ni magumu sana, hata hilo lazima serikali ya shirikisho, hatua za kuifikia ni hatarishi kwa muungano huu.
Simplicity is the sense of Intelligence,its a matter of reading between the lines.
 
Kabudi huwa anajisikia sana!! Ana arrogance ya usomi ambayo namuonaga kama mtu wa hovyo hovyo!! Kuna vitu huna haja ya kuvielezea kwa kujitapa ili mkubwa akupende kwani huwa vinazaa mambo mengine amabayo huwa yanaleta taharuki!!!

Hii kuwachukua watu vyuoni na kuja kuwapa madaraka ya kiutendaji ina madhara sana!! Yeye alifikiria anafanya lecture ya constitutional law kumbe anaongea na watanzania wote. Bungeni sio darasani kabudi jiongeze!!!
Ni kweli...jinsi anavyoongea ni kama anafundisha....papala nyingi sana ili usomi wake uonekane...kuna vitu vya kutumia hekima na akili tu...ili kuepusha shari na maisha yaende..alikosa hekima nzuri ya kupresent hoja yake...
 
Dah! Kwahiyo mtakwenda kuwauwa?

kwani wanalalamika lini? Muungano miaka yote uba mambo haya haya, alichosema kabudi ni tafsiri sahihi

kama hawana jeshi hawana chochote wanaweza kufanya

sasa tafsiri yako ya eti tutawaua, ndio ulichowaza hicho? na wewe una tatizo kabla haujanywa unakuwa msumbufu
 
Hatupendi ukweli, ila ukweli ni kuwa Zanzibar ilipaswa kuwa Mkoa kama ilivyo Iringa au Mbeya.
Tungekuwa na nchi nzuri sana.
Technical ni mkoa tu,Ila theoretical ni nchi lakini siku za usoni naiona zanzibar kama nchi inayojitegemea/inayojitawala yenyewe na kuamua mambo yake.
Muda ni kila kitu
 
Mwisho wa siku alichosema ni kweli?

Ndugu wakati wote mtu anaejua anachokisema huonekana kama mwenye maringo na kujisikia kwa wababaishaji.

Ndoa yoyote ile lazima wote mkubali kupoteza 50% ya uhuru wenu otherwise hakuna ndoa hapo lzm mmoja ajifanye mjinga.

Tanganyika pia imepoteza mengi sana kwenye huu muungano lkn hatulalamiki, Zanzibar chokochoko hizi za kudai yale machache tu waliyopoteza inaletwa na wasioutaka muungano.

Na wanajua ili Zanzibar iyapate yote ya kwake ni muungano usiwepo ndio sasa rais wa Zanzibar akiwa na hadhi sawa na rais wa muungano kuna muungano tena hapo? Wanasahau makamu pia anaiwakilisha Zanzibar wakati sisi hatuna anaetuwakilisha uko kwao.
Kiuhalisia huyo rais wa zanzibar hana tofauti na wakuu wa mikoa
 
Technical ni mkoa tu,Ila theoretical ni nchi lakini siku za usoni naiona zanzibar kama nchi inayojitegemea/inayojitawala yenyewe na kuamua mambo yake.
Muda ni kila kitu

Na hili la Le Professor linaenda kuwazindua wanzanzibar kwa ujuma wao.
 
Rais wa Zanzibar hadhi yake ni sawa na hadhi ya Waziri wa kawaida tu ambaye kimsingi huwa amechaguliwa kwa utashi wa mtu mmoja tu, yaani Rais wa JMT .


...............
Ukisoma hicho alichokiandika hapo juu. Na akiangalia chaguzi zote za Zanzibar zilizofanyika tangia 2005.
Yeye kwa elimu dunia yake anadhani kuna utofauti gani?
Je anamjua Jecha wa ccm?

Sasa kwanza waanze kuheshimu kura za wananchi wa zanziba ndio waje na vinyongo vyao.
(Hapa kwenye mabano kuna tusi la da Mange)
 
Kule ni rahisi zaidi watu kwa watu wakule kurubuniwa ndiko yanakotokea matatizo mengi yakimataifa mfano meli iliyoleta mzozo mkubwa was samaki baadae tunaambiwa kibali kilitoka kule,meli zenye kubeba madawa ya kulevya duniani tunaambiwa kibali kimetoka kule, gaidi mkubwa kakamatwa ughaibuni tunaelezwa ni mzawa was zanzibari..yapomengi hata uthubutu wakuteka ndege ni kulekule hivyo nikama kuna kizazi ambacho nadhani ule utumwa umeacha sio tu kovu baali athari kubwa kw a jamii ile hivyo kusipokuwepo na muungano na tuka Shea uelewa itakuwa ni shida si pale tu Bali sehemu kubwa ya Afrika
 
Lengo la wengi sijalielewa ila kwa mawazo yangu katiba ni kitu kinachorekebishika nadhan ni vyema viongozi wakaliona hilo na kufanya mabadiliko chanya ili tusonge mbele bila kulaumiana,muungano ukivunjika wapo watakaoumia sana kuliko tunavyofikiri,nadhan pia sio busara kushabikia uvunjike ili hali kuvunjika kwake hakukupi faida yoyote! Wakati mwingine ni busara kujiweka katika hali ya watu wengine ili upate hisia halisi.
Wapo viongozi wachache huona muungano ukivunjika wao watapata fursa za kiuongozi hao hawako kwa maslahi ya wengi! Baadhi ya wenye uchungu watizameni na wapimeni katika mengine mtabaini huo utaifa wa kuipenda zanzibar hawana.
Hata kwa upande wa Tanzania bara wapo wanaoonyesha kama wana uchungu na Tanganyika ambayo hawajawahi hata kuiishi,nao tuwapime uzalendo wao ktk mengine ili tutumie muongozo wao katika jambo hili.
Maboresho ya baadhi ya vifungu hayaepukiki ili kuendana na nyakati na kizazi kilichopo na kijacho.
 
Yaani ninachikiona hapa watu tunataka prof nguli kama huyo ambaye ameimarisha wanasheria wengi amung'unye maneno. Kama tunataka mabadiliko badilisheni katuba lakini tusitake prof aseme hisia zetu na sio katiba. Mkibadilisha naye atabadilisha usemi.
Mbona hata Shivj husema WAZI ZNZ SIO NCHI kwa maana ya STATE yeye hufananisha ZNZ na taifa lakini siyo STATE koz DOLA ni JMT sasa mnataka wadanganye au watumie busara kuongea na wakati hapo ni suala la kisheria. Mabadiliko ya usemi yanatakiwa yaanzie ktk KATIBA prof Yuko sawa
 
Back
Top Bottom