Wakili wa ESCROW, Gabriel Mnyele aliyetuhumiwa kumuua mkewe ashinda rufaa

kayogo

Member
Sep 15, 2010
75
42
Tuesday, December 28, 2010 9:48 PM

Mnyele alifutiwa adhabu hiyo mbele ya Jopo la Majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa Jaji Salum Massati, Mbarouk Mbarouk na Benard Luanda baada ya kutengua hukumu ya Mahakama Kuu juzi.

Mahakama ilifuta hukumu hiyo baada ya kuridhika na utetezi wa mawakili wa mrufani huyo kuwa Mahakama Kuu ilikosea kumtia hatiani kwa kuwa
hukumu hiyo iliegemea ushahidi wa mazingira na upande wa mashtaka ulishindwa kuthibitisha tuhuma dhidi yake.

Mnyele alihukumiwa Oktoba 19, mwaka jana na Jaji William Mandia wa mahakama Kuu kwa kosa la kumuua mkewe, Pamela Ngunyali kosa alilokuwa akituhumiwa na kukata rufaa kupitia kwa mawakili wake wanaomtetea,Mabere Marando na Richard Rweyongeza.

Moja ya kasoro zilizobainishwa na mawakili wa rufaa huyo ni kitendo cha upande wa mashitaka kushindwa kuwasilisha mahakamani jalada la
matibabu na kushindwa kuthibitisha chanzo cha kifo cha marehemu, hoja ambayo iliungwa mkono na Mahakama.

Mahakama ya Rufaa ilisema kitendo cha kutokuwepo kwa kumbukumbu za matibabu za marehemu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kilisababisha kutokuwepo kwa kiungo cha ushahidi huo wa mazingira katika kesi hiyo.

"Kwa hiyo tumeridhika kuwa ushahidi wa mazingira kwenye rekodi umeshindwa kukidhi matumizi ya aina hiyo ya ushahidi katika kuthibitisha kuwa ikiwa sababu ya kifo cha marehemu ilikuwa ni majeraha ya kichwani na mrufani ndiye aliyesababisha majeraha hayo," ilisema Mahakama.

"Kwa sababu hizo hapo juu tunaikubali rufani na tunatengua hatia na katika kutekeleza uwezo wetu wa kisheria, pia tunatengua adhabu
iliyotolewa katika Mahakama Kuu," ilieleza hukumu ya majaji hao. Awali, Mahakama ya Rufaa ilisema upande wa mashtaka ulipaswa kuwaita mahakamani mashahidi waliomtibu marehemu katika Hospitali ya Muhimbili, si tu kutoa maelezo ya matibabu, bali pia kuweka wazi
mashaka juu ya chanzo cha kifo cha marehemu.

Aidha, Mahakama hiyo ilisema kuwa hoja nyingine ni upande wa mashitaka kushindwa kushughulikia kitendo cha Dk. Mwakyoma kufika mahakamani bila kuwa na jalada la kumbukumbu za matibabu ya marehemu, kitendo walichodai kuwa ni athari kubwa katika kutenda haki. Akizungumza baada ya hukumu hiyo, Mnyele alisema "nimefurahi sana kuwa haki imetendeka, nimeonekana sina hatia na jina langu sasa limesafishika na namshukuru Mungu kwa yote yaliyopita.

Jambo hili lilikuwa likinisumbua sana maana lilinizuia mambo mengi, lakini sasa nitaingia kwa nguvu katika kugombea ubunge wa Afrika Mashariki." Awali, ilidaiwa kuwa Mnyele alikuwa akikabiliwa na shitaka la kumuua mkewe Pamela Ngunyali kwa kumpiga ofisini kwake katika jengo la Hugo Kinondoni baada ya kugombana.

Ilidaiwa na upande wa mashtaka kuwa Mnyele alimpiga mkewe huyo Novemba 10, 2003 na kumsababishia majeraha ambapo alikimbizwa katika Hospitali
ya Dar Group kabla ya kuhamishiwa Muhimbili ambako alifariki dunia Novemba 20, mwaka huo. Kwa mujibu wa taarifa za daktari, Pamela alifariki dunia kutokana na majeraha ya kupigwa kichwani, lakini Mnyele katika utetezi wake alisema hakumpiga, bali alijikata kwenye mlango wa vioo ofisini kwake wakati alipotaka kumpiga teke.


Chanzo: Nifahamishe
 
Nimemwona #MARANDO wa chadema humo akifanikisha jitihada za kuwadididmiza maiti na wanyonge wasio na hatia.

Halafu kwenye majukwaa wanailaumu CCM nq makuwadi wake kuwa wanawanyonga watanzania kupata hakhi yao ya msingi.

This is TANZANIA MASLAHI. NOT IMANI.
 
Hii nchi hakuna mwenye uchungu nayo, hata wale wanaolia ni sababu tu wamekosa mshiko. Nilimuuliza jamaa yangu mmoja aliyekuwa akilalamika sana kuhusu escrow nikamwambia deep from your heart, ingetokea ukakuta hela ya escrow kwenye akaunti yako ungeirudisha? Kwa uungwana kasema hangeweza!!
 
anazipata wapi nguvu hizi za kuwahadaa majaji wa nchi hii gabriel mnyele?
 
Salum Massati, Mbarouk Mbarouk na Benard Luanda hawa majaji sidhani kama wana credibility ya majaji bora Tanzania. Masati ni vituko vitupu, tunamkumbuka katika kesi ya wahanga wa madini. Hukumu yake ilikuwa very controversial! Imeweka historia ya jaji controversial
 
Hats huyo lissu tundule; mi naona ni mnafiki tu alikuwa wapi kusema siku zote. Eti Leo ndo aseme. Mawakili ndo kazi zao; kuutetea uongo use kweli and vice versa.
 
Hats huyo lissu tundule; mi naona ni mnafiki tu alikuwa wapi kusema siku zote. Eti Leo ndo aseme. Mawakili ndo kazi zao; kuutetea uongo use kweli and vice versa.

Tundu Lissu alikuwa anajibu tuhuma toka kwa mbunge mmoja wa ccm aliedai wakili aliedai kwamba wakili aliefungua kesi jana ni mjumbe wa kamati kuu Chadema..
 
[QUOTE"nyumba kubwa, post: 19470413, member: 27679"]ameshajiuzuru[/QUOTE]

Naona vetting haikufanyika vyema hapo awali. Kiongozi mkuu kama yeye hapaswi kuwa na doa kama alilokuwa nalo huyu X-DC
 
Back
Top Bottom