Wakili Robert Amsterdam ni nani?

Wakili Robert Amsterdam ni nani?

Baada ya taarifa za kuwepo kwa Tweet yenye barua ya wazi toka kwa raia wa Canada Bw. Robert Amsterdam, nimelazimika kujielemisha ili kujua huyu mtu ni nani, thanks to Google search. Niliyosoma kuhusu huyu mtu yamenishitua.

Kwa kifupi imeelezwa kwamba Bw Amsterdam ni wakili wa kimataifa anayejihusisha na kesi za kisiasa, mikataba ya madini, haki za binadamu, uwakilishi wa kisheria wa makubwa duniani, n.k.

Kati ya kesi maarufu alizowahi kuzisimamia wakili Amsterdam ni zile zilizo wahusisha tajiri Mikhail Khodorkovsky wa Urusi na bilionea Thaksin Shinawatra wa Thailand. Wote hawa walishitakiwa nchini mwao kwa tuhuma za uhujumu uchumi na kuonyesha nia ya kupindua serikali za nchi zao. Ni wazi kwamba Rais Putin wa Urusi hakuchelewa kumsweka ndani tajiri huyo wa mafuta.

Kwenye kichwa cha habari "A lesson in Intellectual dishonesty and International meddling" mwandishi wa habari Tony Cartalucci anaelezea Wakili Robert Amsterdam kama mtetezi wa majambazi (convicted criminals) hida ya serikali kwa kutumia agenda za Uhuru wa kisiasa.

Wakili Amsterdam pia ameshiriki kwenye kesi za mikataba ya madini katika nchi za kiafrika. Kama raia wa Canada sitashangaa nikisikia kwamba pia alihusika kusimamia makampuni kama Acacia kwenye kesi mbali mbali za kuishitaki Tanzania kwenye mahakama za kimaifa.

Huyu ndiye mtu ambaye Tundu Lissu amemkodisha kusimamia kwenye shughuli zake za kisiasa. Swali linakuja akilini ni kwamba Bwana Lissu amempa ahadi gani ikiwa atakupa Rais?

Huyu mtu anahesabu za political goes gani kwa Tanzania kama ilivyokuwa huko kwenye mataifa mengine? Hakuna chembe ya ukweli kwamba mkataba wa Bw Lissu na Amsterdam unahusu kutuma ya kisiasa.

Andiko la mwandishi Tony kuhusu Intellectual dishonesty and International meddling linatoa picha kamili ya huyu mtu. Hapo ndipo Mh. Lissu ametufikisha kama nchi.

Nadhani kuna ukweli kwamba anatumwa na wakubwa.
Mzee mmoja wa nchi ya ulaya, shoga, kachanganyikiwa, msambazaji wa imani ya ushoga, anatafuta umaarufu, kajichokea, hana la kufanya zaidi anatafuta kiki ya ya kujiona au kuonekana anafanya cha maana duniani, tumpuuze tu...
 
Kabla ya kuingilia siasa za Tanzania ni vyema ndugu Robert Amsterdem amshawishi Rais Erdogan wa Uturuki kuwaachia wafungwa wa kisiasa zaidi ya 80,000 waliopo kizuizini huko uturuki.

Rais Magufuli hajaweka kifungoni hata mwanasiasa mmoja as we speak.

ni vyema mfanyabiashara huyu akawa na hulka ya kusimama katika haki.

ajiulize kwanza haki ya raia wa uturuki wakiwemo wanajeshi,walimu n.k ipo wapi huko uturuki?

Kwa upande wa mshirika wake hapa Tanzania je anaridhia raia wa uturuki zaidi ya 80,000 kuendelea kukaa lupango?kama ni hivyo yeye anatarajia kufunga watu wangapi?
Mods mliunganisha hii thread yangu ..nimepata tabu kuisaka
 
Bwa mdogo hebu tulia acha legends tukupe vitu
Legend enzi zako zimepita hizi ni za malegendary wa viwango vyako vya enzi hizo kama akina Mwashambwa,Tlatlaah,choice variable na chawa wafananao.
 
Legend enzi zako zimepita hizi ni za malegendary wa viwango vyako vya enzi hizo kama akina Mwashambwa,Tlatlaah,choice variable na chawa wafananao.
wote hao wamenikuta na wakaniacha
 
Kabla ya kuingilia siasa za Tanzania ni vyema ndugu Robert Amsterdem amshawishi Rais Erdogan wa Uturuki kuwaachia wafungwa wa kisiasa zaidi ya 80,000 waliopo kizuizini huko uturuki.

Rais Magufuli hajaweka kifungoni hata mwanasiasa mmoja as we speak.

ni vyema mfanyabiashara huyu akawa na hulka ya kusimama katika haki.

ajiulize kwanza haki ya raia wa uturuki wakiwemo wanajeshi,walimu n.k ipo wapi huko uturuki?

Kwa upande wa mshirika wake hapa Tanzania je anaridhia raia wa uturuki zaidi ya 80,000 kuendelea kukaa lupango?kama ni hivyo yeye anatarajia kufunga watu wangapi?
Hakuweka wanasiasa kifungoni ???

Nikuongeze pia alitengeneza wakimbizi wa kisiasa wengi kwa mara ya kwanza kuzidi hata awamu ya kwanza.
 
Back
Top Bottom