Madai
Julai 15, 2025 ziliibuka taarifa zikieleza kuwa wakili Robert Amsterdam amejitoa kuisimamia CHADEMA katika kesi zake kwa sababu ya deni la Dola 20,000. Taarifa hiyo imeambatana na grafiki yenye utambulisho wa The Chanzo.
Pamoja na hiyo ipo pia taarifa nyingine ikieleza kuwa Mwanasheria mkuu wa CHADEMA, Dkt. Rugemeleza Nshala amethibitisha kuwa ni kweli Amsterdam wamejitoa kusimamia kesi zao zote.
Uhalisia wa madai hayo
JamiiCheck imefuatilia taarifa hizo na kubaini kuwa
si za kweli.
Juni 26, 2025 CHADEMA ilitoa taarifa kuujulisha Umma kuwa kampuni ya kisheria ya Amsterdam and Partners LLP yenye makazi yake Marekani na Uingeresa kuwa itakuwa ikisimamia kesi zinazokikabili chama chama hicho pamoja na ushauri wa kisheria.
Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck kwa njia ya mtandao na katika kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya
Robert Amsterdam pamoja na wa
Kampuni ya Amsterdam imebaini kuwa hakuna uthibitisho unaothibisha taarifa hiyo.
Aidha Julai 15, 2025 kupitia
ukurasa wake wa X Robert Amsterdam alilandika;
“Wale wanaosimamia uchaguzi nchini Tanzania waelewe kwamba wameufanya mchakato huo kuwa batili na usio na thamani kabisa. Wanafungua milango ya kuwekewa vikwazo na kulaumiwa vikali na jumuiya ya kimataifa.”
Aidha hakuna taarifa yoyote kutoka
CHADEMA inayoleza kuwa wameachana na Mwanasheria huyo pamoja na kampuni yake.
Grafiki zilizotumika kusambaza Taarifa hizo ni za kughushi kwani hazijatolewa na vyanzo hivyo kama inavyoonekana