Wakili Peter Kibatala: Rufaa ya Lissu kuna mambo elfu moja ya kusema

Wakili Peter Kibatala: Rufaa ya Lissu kuna mambo elfu moja ya kusema

Atukuzwaye

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2026
Posts
252
Reaction score
402
Wakili Kibatala, amesisitiza umuhimu wa vyombo vya utoaji haki nchini kutenganisha kwa uangalifu dhana ya kutokuendeshwa na shinikizo la mtaani huku vikizingatia maoni na matarajio ya jamii ili kuepusha mifumo ya kisheria kujitenga na wananchi. Aliyasema hayo alipokuwa akizungumza pembezoni mwa mazishi ya Mzee Alute, ambaye ni kaka wa mwanasiasa mkongwe Tundu Lissu.

Akizungumzia hatua zinazofuata za kisheria, Wakili Kibatala alieleza kuwa mipango na mikakati ipo tayari kwa ajili ya kupeleka shauri hilo katika Mahakama ya Rufaa endapo atapata nafasi ya kushiriki katika mchakato huo, akisisitiza kuwa mahakama ndiyo jukwaa sahihi na lenye mamlaka ya kubadilisha maamuzi yaliyotolewa hapo awali. Aliongeza kuwa wakati wa msiba na hali ngumu kama hiyo, nidhamu ya kisheria na kusubiri maelekezo ndiyo njia sahihi ya kufuata badala ya maneno yasiyo na tija nje ya utaratibu.

Aidha, akigusia hisia za wananchi na hali halisi mtaani kuhusu mifumo ya haki, alieleza kuwa utoaji haki hufanyika kwa niaba ya jamii, hivyo ni lazima matendo ya vyombo vya sheria yaakisi kile kinachotazamiwa na wananchi. Alibainisha kuwa ingawa watoa haki hawapaswi kuendeshwa na mihemko ya mtaani, ni muhimu kuwepo na uwiano mzuri ili kuzuia vyombo hivyo kujitenga na jamii, jambo ambalo linaweza hatimaye kusababisha mfumo mzima wa kisheria na kijamii kuanguka.

Mwishoni mwa kauli yake, Wakili Kibatala alihitimisha kwa kusema kuwa lengo kuu la michakato yote ya kisheria ni kuhakikisha haki inatendeka ipasavyo na wananchi wanapata msaada stahiki ili waweze kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa. Alisisitiza kuwa msimamo huo ndio utakaowaongoza katika hatua zote za rufaa pindi watakapopata fursa ya kushiriki rasmi katika mchakato huo.

Wewe mdau una lipi la kusema juu ya kauli za Kibatala?

 
Wale wa matusi mengi hawawezi kuelewa, na wale wanaharakati wa mtandaoni watasema asali imemuelemea.

Wengine wanaweza tafsiri ni kundi moja na Lema.

Ngoja tuone matusi yatakayo tukanwa.
 
Kuchomoka ni ngumu sana wanabishana na jambo ambalo sheria imeweka wazi tena imefafanua kwa kina sana.Mdomo uliponza kichwa kila siku tunaambiwa chunga mdomo wako CDM wao hawasikii.
 
Kuchomoka ni ngumu sana wanabishana na jambo ambalo sheria imeweka wazi tena imefafanua kwa kina sana.Mdomo uliponza kichwa kila siku tunaambiwa chunga mdomo wako CDM wao hawasikii.
Na huyu aliyesema hakuna nywinywinywi alikuwa sahihi na akaamrisha jeshi?
 
Back
Top Bottom