GE2025 Wakili Olengurumwa: Amani ya nchi inalindwa kwa uwepo wa Misingi ya Demokrasia na Kusikiliza kero na Vilio vya Wananchi

GE2025 Wakili Olengurumwa: Amani ya nchi inalindwa kwa uwepo wa Misingi ya Demokrasia na Kusikiliza kero na Vilio vya Wananchi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Wakili Onesmo Olengurumwa, Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), amesema kuwa msingi wa kulinda amani ya nchi upo katika kujenga na kuimarisha misingi ya kidemokrasia na usawa wa kijamii na si vinginevyo

  • Akizungumza na mtangazaji Wilberforce Ngoto katika kipindi cha Maswali na Majibu cha Jambo TV, Olengurumwa amesema amani hudumu endapo wananchi wanashirikishwa ipasavyo katika maamuzi ya nchi, haki za makundi yote zinaheshimiwa na rasilimali za taifa zinatumika kwa usawa

“Amani ya nchi inalindwa na uwepo wa misingi ya kidemokrasia. Inalindwa na uwepo wa sheria, na inalindwa kwa kuhakikisha haki za makundi yote zinaheshimiwa. Amani inalindwa pale ambapo kuna usawa katika matumizi ya rasilimali za taifa, na wananchi wanashirikishwa kikamilifu katika nafasi za uongozi na maamuzi ya nchi yao. Amani inalindwa pia pale ambapo serikali inasikiliza kero na vilio vya wananchi, na kuzifanyia kazi kwa dhati. Ukipuuza haya, huwezi kulinda amani”, amesema Olengurumwa

Soma pia

 
Back
Top Bottom