PreGE2025 Wakili Jebra: Hatutegemei visingizio vyovyote Lissu kutoletwa Mahakamani Mei 19, 2025

PreGE2025 Wakili Jebra: Hatutegemei visingizio vyovyote Lissu kutoletwa Mahakamani Mei 19, 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Wakili Jebra Kambole, mmoja wa mawakili wa utetezi wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu, amesema kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru kesi ya mteja wao isikilizwe kwa uwazi kuanzia Mei 19, 2025.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Jumatano Mei 14, 2025, Jebra amesema:

"Kama mtakumbuka siku ta tarehe 06/05/2025 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilitoa amri ambayo ilikua inatoa mambo kadhaa (kuhusiana na kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Lissu), tumewaita kuffanua amri hizo ni amri zipi ambazo Mahakama ilizitoa, kwanza Mahakama ilitengeua amri yake ya mwanzo ya kusikiliza shauri hili kwa njia ya mtandao ambapo katika kutengua huko Mahakama ilitoa amri kwamba shauri hili litasikilizwa kwa njia ya wazi, ilitoa amri kwamba kesi hii itasikilizwa kwa Mahakama ya wazi na ilitoa maelekezo kwamba itasikilizwa chumba namba moja katika Mahakama ya Kisutu hivyo tarehe 19/05/2025 itasikiliza hoja za awali zinazohusu kesi ya uchochzezi."

"Mahakama ilitoa amri kwa maafisa wa Magereza hapa namaanisha kwamba Mahakama ilitoa amri kwa Mkuu wa Magereza kuhakikisha tarehe 19/05/2025 Lissu analetwa, hivyo hatutegemei visingizio kwamba gari, bovu, sijuwi kwamba foleni, kiujumla hatutegemei visingizio vyovyote vinavyoweza kusabisha mteja wetu kuletwa Mahakamani, ikiwa Mahakama ya wazi umma unaruhusiwa kushiriki, kwa hiyo Mahakama ilisema kwamba Mahakama inawaalika au inawaomba kuhudhuria, kwa hiyo watu wasikae nyumbani au wasisite kuja kwa sababu Mahakama imeshatoa amri hiyo."
 
Na huyu Dr cossey aliemtisha fr kitima kwamba atashughulikiwa mbona afikishwi mahakamani.?!
download (2).jpeg
 
Hivi itarushwa kwenye TV?maana nilimsikia Mkurugenzi wa Sheria Dr.Nshala anasema kwamba itakua ya kihostoria na itarushwa live kama nchi zingine
 
Back
Top Bottom