Wakili ataka maombi ya Mtikila yatupwe

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,083
Mtikila%2815%29.jpg

Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila.



Wakili Alphonce Katemi anayemtetea mdai Paskazia Matete, ameiomba mahakama kutupilia mbali maombi ya kulipitia upya shauri la madai ya deni la Sh. milioni 9.8 anazodaiwa Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila pamoja na Mariamu Issa.
Anaomba shauri hilo litupwe kwa madai kwamba hoja za Mtikila ni za uongo na zinalenga kuipotezea muda mahakama.
Wakili Katemi alitoa madai hayo na kumuomba Hakimu Mkazi, Joyce Minde wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam kukazia amri ya uuzwaji wa mali nyingine za Mtikila kufidia deni hilo kama hukumu ilivyotolewa awali.
Aidha, Katemi alidai maombi ya Mtikila yalitakiwa kutolewa ndani ya siku 30, lakini yakapelekwa nje ya muda huo na kwamba, mdaiwa alifahamu hilo na hakuwasilisha sababu za msingi mahakamani.
Mtikila alidai aliwasilisha maombi mahakamani kutaka kesi hiyo ipitiwe upya kabla ya kuchukua maamuzi yaliyotolewa katika hukumu kuwa mali zake zikamatwe na kuuzwa ili zifidie deni hilo, kwa madai kwamba wakili wake alijitoa bila kumuarifu.
Hukumu hiyo iliyotolewa na Hakimu Kibona mahakamani hapo, iliamuru pia endapo zoezi hilo litashindikana, basi ombi lililotolewa na mdai kutaka Mtikila afungwe kifungo cha madai cha miezi sita gerezani kitatekelezwa.
Hukumu hiyo ilitolewa baada ya kuwapo pingamizi lililowekwa na mdai Kampuni ya Kimataifa ya CIELMAC iliyotaka kusitishwa mnada wa kuiuza nyumba iliyoko kiwanja namba 273 Block “C” Mikocheni, yenye hati namba 186311/ 37, iliyodaiwa kuwa ni ya Mtikila.



CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom