Kwa kweli inashangaza kuona wachangiaji wakijadili kwa jazba wakati hata alichosema Msando kwenye hicho kipindi hakijawekwa hapa. Jamani tupunguze mihemko na tujenge utamaduni wa kujadili hoja. Kwa nini tusijadili alichokisema badala ya nani zaidi kati ya Msando, Zitto, na Lissu? If anything, njia nzuri ya kuonesha ni nani zaidi ni kuchambua hoja zao na kuweka wazi hoja dhaifu. Kusema tu fulani anamzidi mwenzake kwa hoja bila kuchambua hoja zao hakusaidii chochote na ni upunguani.