Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 8,273
- 25,303
Idadi ya Wakenya wanaoingia Tanzania kwa kuhofia fujo ikizidi kuongezeka. Mwananchi ilikuwa katika vijiji vilivyo jirani na mpaka wa Horohoro mkoani Tanga na kukuta idadi ya wanaovuka kutoka Kenya kuingia Tanzania kuwa kubwa ikilinganishwa na siku ambazo si za uchaguzi.
Mwanakombo Ali ambaye ni Mkazi wa Vanga nchini Kenya amesema amelazimika kuondoka kutokana na hofu kwambahuenda siku ya uchaguzi ikatokea vurugu.
“Mimi na watoto wangu watatu tumekuja hapa Duga Maforoni kwa baba
yangu,huku ndiko nyumbani kwetu na Vanga ni kwa mume wangu kwani hivyo
nimeona nising’anganie kukaa mahala ambapo tunaweza kuuawa ikitokea
vurugu”amesema Mwanakombo.
Salehe Mohamed amesema katika kijiji cha Mwakijembe wilayani Mkinga mkoani Tanga kuwa yeye ni mkazi wa Mombasa nchini Kenya na alikuwa amejiandikisha kupiga kura lakini kutokana na hofu ya kutokea vurugu ameamua kuondoka yeye na familia yake ili kuokoa maisha.
“Tutakaa hapa hadi uchaguzi utakapofanyika na kutajwa mshindi kwani hali si shwari kwa sasa hivi akishinda Uhuru kutatokea vurugu na hata akishinda Odinga kutatokea vurugu tu”amesema Salehe.
Katika mapaka wa Kenya na Tanzania,Mwananchi ilishuhudia abiria wanaoingia Tanzania kupitia mabasi ni kubwa kuliko wanaokwenda Kenya.
Ambapo wengi wao ni raia wa wa Kiasia na kutoka nchi za Ulaya.Ofisa mmoja idara ya uhamiaji katika ofisi ya Horohoro ambaye hakutaka.
Jina lake litajwe amesema kumekuwa na idadi kubwa ya abira wanaopitakatika mpaka huo wakitokea nchini Kenya kuingia Tanzania na sababu ni kutokana na uchaguzi.
Chanzo: Mwananchi