Tigga Mumba
JF-Expert Member
- Nov 18, 2010
- 746
- 474
Nawasalim,
Ninadhani hii topic ilishakuja mara kadhaa lakini nashare nanyi hii kitu inayonifanya nikose raha sana nyumbani.
Tuna wiki sasa amekuja msichana mdogo wa kazi kwa ajili ya kusaidia pale nyumbani. Mke wangu anamkosoa huyu dada kwa kila jambo tena kwa ukali. Mara nyingine naona kabisa anamuonea lakini kuingialia hapo ni ugomvi usioisha.
Pia nimegundua mke wangu kama ana pressure hivi kuhusu huyo dada. By the way ni dada mdogo 18yrs ametoka kijijini Iringa, hata kufungua mlango wa fridge alikuwa hajui, amefundishwa siku mbili tatu.
Tatizo hasa kwa akina mama ni nini? Mfano nimemshauri mke wangu amuandalie ratiba ya siku na kazi za kufanya zile fixed. Sababu tunaishi watatu tu kwa sasa, kazi si nyingi. Yeye atamuamsha saa kumi na moja asubuhi na usiku mpaka asubirie tule atoe vyombo ndio akalale!!
Amani imepotea kiasi ndani nyumba. Kwa wenye experience naomba tushirikishane, je ni approach gani nzuri niitumie ili kila mtu awe na amani nyumbani. Amani namaanisha dada wa kazi ajisikie kama mtu anayethaminiwa na mke wangu asione kama mimi nina mawazo mabaya(ngono etc) kwa dada au asione kama nampendelea dada**.
Ongea na mkeo kwa upendo amfundishe huyo bint taratibu kwa upole.pia ahakikishe bint anapata muda wa kupumzika mchana na usiku alale mapema.kama ana tabia njema hamtajuta.nina wa kwangu nilimpata alikua hajui chochote nikafanya hivyo ni mwaka wa nne ninae na hana ukorofi.Kuna baadhi ya watu huna na mawazo kuwa house girl ni kijakazi, hastahili hata kula chakula mnachokula ninyi. Mweleze mkeo kuwa amshukuru mungu kwa kumpa wazazi wwaliokuwa na uwezo na kumpatia elimu. Huyo house girl ametoka kijijini huenda hata friji ndio kwanza kalionea hapo, sasa ni wajibu wa mke wako kumfundisha, asifikiri shule ni mpaka uende darasani.
Labda nikuulize swali la kiuchokozi, huyu msichana wa kazi nani alimtafuta, wewe au yeye? Na hii tabia ni kwa msichana huyu tu au kwa wasichana wote uliowahi kukaa nao?
Mkeo anafanya hivyo kwasababu anawasiwasi na wewe , Maaana nyie wanaume huwa hamueleweki kuhusu wasaidizi wa ndani,Pia mimi nafikiria kaa na mke muelekeze ama mshauri kuhusu kuishi na huyo binti, pia muhakikishie kuwa asiwe na wasiwasi na wewe juu ya binti wa kazi.Vilevile yeye Mama ndiye anayetakiwa kuwa karibu na binti kuliko wewe.
Pindi anapomfokea ama kumgombeza wewe usingilie, waache ila pembeni mwite mkeo umueleweshe usimgombeze mkeo mbele ya binti.
mna watoto? kama ndio, wa umri gani?
Nawasalim,
Ninadhani hii topic ilishakuja mara kadhaa lakini nashare nanyi hii kitu inayonifanya nikose raha sana nyumbani.
Tuna wiki sasa amekuja msichana mdogo wa kazi kwa ajili ya kusaidia pale nyumbani. Mke wangu anamkosoa huyu dada kwa kila jambo tena kwa ukali. Mara nyingine naona kabisa anamuonea lakini kuingialia hapo ni ugomvi usioisha.
Pia nimegundua mke wangu kama ana pressure hivi kuhusu huyo dada. By the way ni dada mdogo 18yrs ametoka kijijini Iringa, hata kufungua mlango wa fridge alikuwa hajui, amefundishwa siku mbili tatu.
Tatizo hasa kwa akina mama ni nini? Mfano nimemshauri mke wangu amuandalie ratiba ya siku na kazi za kufanya zile fixed. Sababu tunaishi watatu tu kwa sasa, kazi si nyingi. Yeye atamuamsha saa kumi na moja asubuhi na usiku mpaka asubirie tule atoe vyombo ndio akalale!!
Amani imepotea kiasi ndani nyumba. Kwa wenye experience naomba tushirikishane, je ni approach gani nzuri niitumie ili kila mtu awe na amani nyumbani. Amani namaanisha dada wa kazi ajisikie kama mtu anayethaminiwa na mke wangu asione kama mimi nina mawazo mabaya(ngono etc) kwa dada au asione kama nampendelea dada**.
Kuna watu wanaona hg kama mnyama vile or what na hawawezi kuishi na mahosegirl vizuri na huku wanataka wafanyiwe kazi.
But inaonyesha wewe na mkeo ni wavivu, unless mniambie kuna sababu ya maana iliyowafanya mchukue house girl. kama nimekusoma mpo watatu ukiongeza house girl. Sioni sababu house girl awe gumzo wakati kama kazi zenyewe ni za kupika na kusafisha. Ondoeni housegirl, kazi hizo ni ndogondogo zifanyeni wenyewe mtakuwa na amani.
Dawa ni kumtarasua huyo house girl mambo yake sawa............................!:tape2:
Watoto bado, tunatarajia(mama kijacho)
Wewe una matatizo ndio maana huyo unaemuita mke wako amekuchoka sasa anakutafutia tu sababu!