Wake wa viongozi wafanya dua ya kuliombea taifa

Wake wa viongozi wafanya dua ya kuliombea taifa

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,923
Reaction score
6,557
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sixtus Mapunda amepongeza chama cha wake wa viongozi Ladies of new millennium group kwa kuandaa dua maalumu ya kuliombea taifa amani na utulivu kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari Sixtus amesema jambo walilolifanya ni jambo kubwa lenye mustaqabali mzuri kwa taifa taifa kwani amani ni kitu muhimu sana nchini.

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha wake wa viongozi cha ladies of new Millennium group ambao ndio waratibu wa tukio hilo Bi Tunu Pinda amesema lengo na dhumuni la kuandaa tukio hili ni kuombea taifa liendelee kuwa na amani na utulivu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu sambamba na hilo wametoa pia sadaka ya vitu mbalimbali ikiwemo michele , taulo za kike Kwa watoto yatima walijitokeza kuliombea dua taifa.

 
Back
Top Bottom