Wakazi wa Tabata Segerea hawana soko

Boran Jakutay

Senior Member
Apr 8, 2023
110
255
Ukiangalia kwa sasa Tabata ni eneo linalokuwa kimakazi kulinganisha na miaka kadhaa nyuma.

Idadi ya watu inaongezeka kila kukicha huku huduma za kijamii zikibaki vilevile.

Ukichukulia mfano Tabata Segerea, hakuna soko lolote, sio soko la vyakula wala mavazi.

Hali hiyo inafanya wafanyabiashara kukitumia Kituo cha Dadadala cha Tabata Segerea Mwisho kuweka bidhaa zao mbalimbali ambazo ni kero kwa abiria na magari.

Kituo cha Daladala kinachukua magari tofauti yanayokwenda Mbezi, Chanika, Kawe, Makumbusho, Kariakoo, Temeke na Kinyerezi, hapo unapata picha gani namna magari yalivyo mengi halafu kituo kimegeuzwa soko.

Sehemu za abiria kusubiria magari na sehemu za kupita kwa watembea kwa miguu ndipo biashara zimepangwa. Watu wanalazimika kupita yanapopita magari kitu ambacho ni hatari.

Licha ya kwamba usafi unafanyika, lakini kuna haja ya kutenga eneo la soko na kituo cha daladala, vitu hivi viwili haviwezi kuwa sehemu moja kama ilivyo sasa. Kiukweli sio sawa.

IMG_20230408_174205.jpg
IMG_20230408_174518.jpg
IMG_20230408_174458.jpg
 
Back
Top Bottom