Invisible
Robot
- Feb 26, 2006
- 16,285
- 8,467
Si siri kuwa mwanadamu anapokosa umeme (katika dunia ya sasa) hulalamika na kuona kama kila kitu kimekwama. Hii ni kwa wale ambao wanaishi mijini ambapo wanapata umeme... Ni kweli, sote tunaihitaji nishati hii ili kuweza kuyasukuma maisha kwa urahisi zaidi.
Lakini linapokuja suala la kuangalia uhai wa mwanadamu huwezi kuacha kuyaongelea "Maji". Yanapokosekana maji (hususani katika nchi za kiafrika) kila kitu kinakwama, wanadamu wanaweza kufa kwa kukosa maji tu, wanyama, mimea na viumbe vyote vinategemea kwa kila hali uwepo wa maji. Ni maji hayahaya yamepelekea Tanzania kuingia kwenye mgawo wa umeme ambao sasa unalitesa Taifa mara kwa mara (pamoja na kuharibika kwa mitambo yetu chakavu).
Sina dhamira ya kuandika ngonjera nyingi hapa, nielekee kwenye pointi yangu moja kwa moja. Jiji la Arusha lina wabunge wengi wenye majina makubwa na hivyo natarajia kilio hiki watakisikiliza na kuchukua hatua za makusudi kuwaokoa wananchi hawa.
Wananchi wa Loliondo kwa sasa wana wakati mgumu SANA kwani maisha wanayoishi yako chini ya dola moja kwa siku (Tshs 1,300/=) na bado wanakabiliana na mtihani mgumu katika maisha wa kununua ndoo moja tu (lita 20) ya maji kwa Tshs 1,000/=.
Siamini kuwa serikali imeshindwa la kufanya kuwaokoa watanzania hawa wachache (hawafikii hata milioni moja) katika janga hili.
Kila mmoja anafahamu athari ya kukosa maji, kila mmoja wetu anajua ni namna gani akikosa maji atakuwa... Watanzania wenzetu wanateseka sana!
Kuna kila dalili kuwa msaada wa haraka usipopelekwa eneo hili watanzania hawa wataanza kufa mmoja baada ya mwingine pamoja na mifugo yao.
Wanaume wa kimasai sasa wanaanza kuzikimbia familia zao na kuwaacha wake na watoto zao wakiteseka. Serikali kama ina dhamira ya kweli kuwalinda raia wake naisihi sana ipeleke msaada eneo hili.
Heri nimesema!