Wakazi wa Kipawa waliohamia Pugu wakatwa na mapanga

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,320
33,125
Masoud Masasi

VITENDO vya chuki vimeendelea kushika kasi katika eneo la Pugu Mwakanga jijini Dar es Salaam kati ya wenyeji na wakazi wa Kipawa waliohamia katika eneo hilo, baada ya Elisante Kawiche kukatwa na panga mkononi.

Tukio hilo, lilitokea juzi saa 11:00 jioni baada ya mwenyeji wa eneo hilo, aliyetambulika kwa jina moja la Frank na wenzake wawili kudaiwa kumvamia Kawiche aliyehamia kutoka Kipawa na kumshambulia kwa mapanga bila sababu yoyote.

Wakizungumza na Mwananchi watu walioshuhudia tukio hilo, walidai watu hao, waliokuwa na mapanga na majembe walifika eneo alikokuwa amepumzika Kawiche na majirani zake na kumshambulia kwa mapanga na kumjeruhi katika kiganja cha mkono na mfupa wake kutoka nje.

?Sisi tulikuwa tumekaa, ghafla akaja kijana mmoja na wenzake watatu na kuanza kumshumbulia kaka Kawiche kwa panga hali iliyofanya tuanze kupiga kelele,?alisimulia Beatrice Mashambo.
Alisema baada ya kumshambulia Kawiche, watu hao walikimbilia kusikojulikana na hivyo walilazimika kumpeleka majeruhi huyo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa matibabu.

?Kwa kweli kaka tulipata taabu kufika hospitalini kutokana na umbali kati ya Pugu Mwakanga na Muhimbili, nadhani mwenyewe umeshuhudia umbali uliopo na mjini,?alisema Mashambo.
Akizungumza na gazeti hili mke wa Kawiche alisema kumekuwa na chuki kati ya wenyeji wa eneo hilo na wakazi waliohamia eneo hilo kutoka Kipawa ambako wamepisha upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere.
Alisema chanzo cha uhasama huo ni wakazi hao kufukuzwa eneo hilo kwa kuwa hawana hati miliki na serikali kuwapa wahamiaji eneo hilo.
Alisema wamekuwa wakiishi kwa uhasama na kwamba walipoanza ujenzi wa nyumba yao, matofali yao yaliharibiwa kwa kuvunjwa vunjwa na watu wasiojulikana.
? Hawa wenyeji waliuziwa kienyeji viwanja hivi, sasa sisi tulivyoletwa huku na serikali ndio uhasama umeanza, hasa eneo hili la block N ndio lina matatizo zaidi,?alisema Mama Kawiche.

Baadhi ya wakazi hao, wameiomba serikali kuingilia kati suala hilo kwa kuwa vitendo vya chuki vinaongezeka kila kukicha na hivyo hali hiyo kutishia maisha yao.

? Mimi naiomba serikali kuingilia kati suala hili, isije ikatokea kama ya wenzetu kule Musoma kwa sababu mtu akipigwa leo, kesho na sisi tutapiga mtu,?alisema mkazi mmoja ambaye alikataa kutaja jina lake.

Wakazi hao waliomba serikali iwapelekee huduma muhimu, ikiwemo kituo cha polisi na zahanati kutokana na eneo hilo kukosa huduma hizo.
Walisema wamekuwa wakitembea umbali mrefu kwenda kwenye zahanati.
?Huku tumeletwa kama wanyama kwa sababu hakuna huduma muhimu kama kituo cha polisi na zahanati unaiomba serikali ituletee huduma hizo,?alisema Saidi Selemani.

Gazeti hili lilishuhudia polisi wakianya doria katika eneo hilo, ili kulinda usalama na kuwasaka watuhumiwa wa tukio hilo ambapo pia Mwananchi ilishuhudia watu wawili wakikamatwa na polisi wakihusishwa na tukio hilo.


http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=18578
 
Back
Top Bottom