Wakazi wa Dar es Salaam, manyunyu kidogo tu mnalalamika. Tatizo ni nini?

relis

JF-Expert Member
May 24, 2015
3,188
4,765
Habari wakuu? Nijiuliza inakuwaje wakazi wa DSM manyunyu kidogo kelele JF, huku DSM mvua kubwa tunashindwa kulala, sijui kama kutakucha. Mwingine kaenda mbali anasema kutokana na Radi watoto wamehamia chumbani kwake Kwa hofu nimeshangaa watoto gani hao.

Vijimanyunyu kelele JF, DSM inazalisha wanaume wa aina gani, kama huku Iringa radi inapiga kama umeifuata ilipo lakini husikii watu kulialia humu, matetemeko yanapita mpaka kitanda unakikuta sebuleni hakuna kelele Wala kutilia huruma humu yangu ni hayo tu.
 
Acha mbwembwe dada, ile mvua ilinyesha hapa mpk uaribifu wa mazingira, we unasemaje ni manyunyu?!
kwani hatujui mvua kubwa kupitiliza na manyunyu???
 
Watu akili zao wamewekeza kujidamka kutafuta rizki ya siku. Mvua kidogo tu wanavurugwa maana no mtoko no kula
 
Mwaka jana ilinyesha mvua kubwa sana ya upepo Geita. Ile mvua kuna maeneo iliua watu. Sikusikia popote habari zile. Imargine hata media hazikuripoti. Lakini hawa wenzetu wasitingishwe kidogo tu😅😅
 
Dah! Wakazi wa Dar es Salaam na hasa wanaume aka wanaume wa Dar, wanadeka mpaka basi! Yaani kakitu kadogo tu, tayari kelele nchi nzima!
 
Mwaka jana ilinyesha mvua kubwa sana ya upepo Geita. Ile mvua kuna maeneo iliua watu. Sikusikia popote habari zile. Imargine hata media hazikuripoti. Lakini hawa wenzetu wasitingishwe kidogo tu
Hujatumia akili
 
Habari wakuu? Nijiuliza inakuwaje wakazi wa DSM manyunyu kidogo kelele JF, huku DSM mvua kubwa tunashindwa kulala, sijui kama kutakucha. Mwingine kaenda mbali anasema kutokana na Radi watoto wamehamia chumbani kwake Kwa hofu nimeshangaa watoto gani hao.

Vijimanyunyu kelele JF, DSM inazalisha wanaume wa aina gani, kama huku Iringa radi inapiga kama umeifuata ilipo lakini husikii watu kulialia humu, matetemeko yanapita mpaka kitanda unakikuta sebuleni hakuna kelele Wala kutilia huruma humu yangu ni hayo tu.
Dar ni Jiji la biashara,Shamba letu ni biashara siyo huko kwenu ambako pesa hadi muende Shambani.Huku Mvua ikinyesha biashara hakuna
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom