Wakati Watanzania tukijifanya Kulichukia Zao la Bangi, angalieni jinsi EU na Uganda watakavyofaidika nalo

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Umoja wa Ulaya (EU) hatimaye imeidhinisha bidhaa za Dawa zinazotokana na Bangi zinazotengenezwa nchini Uganda kusafirishwa na kuuzwa katika Masoko.

Chanzo Taarifa: Gazeti la MWANANCHI na Mtandao wao pia

Sasa nyie endeleeni tu Kujifanya mnazuia hilo Zao huku kila Siku mkikimbilia tu Kuchoma Mashamba ya Watu huku mkiwa hamjui kuwa hapo mnapoteza Fedha nyingi sana na ambazo pengine kama nanyi mngeliboresha hilo Zao basi Tanzania ingejipatia Pesa nyingi, Uchumi wake Kukua na hata Maisha ya wale Watanzania wenzetu wanaolima nao Maisha yao yangebadilika na kuwa mazuri.

Kazi Kwenu!
 
Niliwahi kuandika humu kuwa hizi video za akina Afande Muroto akiwa mlimani anafyeka mashamba ya bangi zitakuja kuwa za majuto sawa na wazee wa kisukuma kule Maganzo walivyokuwa wanachezea almasi bao kabla ya wakoloni hawajawapa goroli na kubadirishana nao almasi!
 
Sio kwamba tunaichukia bangi tatizo wavuta bangi lishe duni bangi inawazidi nguvu maarifa na akili end of the day wanafanya vitu vya ovyo
 
Ngoja tusubirie baada ya miaka 5 kama watakuwa salama na sisi tuanze,maana kama nchi zote mbili tukiwa tunatumia bangi halafu halafu wote tukadhurika matokeo yake yatakuwa mabaya sana,hakuna atakayeweza kumsaidia mwenzake...
 
Legalize it..
Kama gongo inaweza kuhalalishwa kwa kuchakachuliwa kisayansi ili kuepuka madhara yake, vivyo hivyo bangi nayo yaweza kuchakachuliwa na kuwa poa kabisa kwa matumizi yetu
 
SLEEPIN GIANT...
bangi milungi haina shida yoyote "special farms products for export only"ubaya upo wapi zaidi mtakuwa mnawakomboa watanzania kwa kujipatia fedha lukuki.
 
Ngoja tusubirie baada ya miaka 5 kama watakuwa salama na sisi tuanze,maana kama nchi zote mbili tukiwa tunatumia bangi halafu halafu wote tukadhurika matokeo yake yatakuwa mabaya sana,hakuna atakayeweza kumsaidia mwenzake...
yaani kinachonishangaza ni watu kuwa wagumu kuelewa Uzi juu!! Bange inayoongelewa ni kwa matumizi ya dawa tu na sio kilevi kama wengi mnavyochangia. Na hata sheria za nchi zote hizo zinapiga marufuku kutumia bange kama kilevi. Kiukweli hii tukiiona kama fursa wakulima Kule tarime wanaweza kunufaika sana tuache kukariri!!!
 
KAma kuvuta bangi siokosa basi mimi sjawahi fanya kosa kabisa
 
Back
Top Bottom