Wakati wa Tanzania kupata Vazi Rasmi la Taifa Umewadia

Baraghash

JF-Expert Member
Dec 18, 2012
2,713
1,789
3-1.jpg

Vazi la Taifa lenye heshima na mvuto na linalo pendezesha watu aina zote limeanza kujitokeza.

Huu ni wakati mwafaka kwa Watanzania kujitambulisha kwa vazi hili ambalo Rais wetu mpendwa kaonyesha njia na limempendeza sana. Vazi hili tayari mshirika mmoja wa Jamhuri ya Muungano, yaani Zanzibar tayari analitumia vazi hili kama vazi lake Taifa. Uzuri wa vazi hili halitumiwi na nchi yoyote duniani kama vazi lao la Taifa.

Vazi hili pia litakuwa na sura ya muungano kama vile picha ya Twiga na Mlima Kilimanjaro inavyoiwakilisha Jamhuri ya Muungano katika Shirika letu la ndege n.k.

NAWASILISHA
 
Nchi ya viwanda , haina haja ya vazi la taifa. Pale unapofanyia kazi na ile nguo ulovaa hilo ndilo vazi la taifa.

Nawasisitiza fanyeni kazi kwa bidii.
 
3-1.jpg

Vazi la Taifa lenye heshima na mvuto na linalo pendezesha watu aina zote limeanza kujitokeza.

Huu ni wakati mwafaka kwa Watanzania kujitambulisha kwa vazi hili ambalo Rais wetu mpendwa kaonyesha njia na limempendeza sana. Vazi hili tayari mshirika mmoja wa Jamhuri ya Muungano, yaani Zanzibar tayari analitumia vazi hili kama vazi lake Taifa. Uzuri wa vazi hili halitumiwi na nchi yoyote duniani kama vazi lao la Taifa.

Vazi hili pia litakuwa na sura ya muungano kama vile picha ya Twiga na Mlima Kilimanjaro inavyoiwakilisha Jamhuri ya Muungano katika Shirika letu la ndege n.k.

NAWASILISHA
Wananchi wanataka bei ya sukari ishuke , hayo masuala ya mavazi sidhani kama yana umuhimu kwa sasa
 
Kwanza Kanzu na Baragashia linavaliwa Sana na Waislamu hivyo ukilianzisha tu kulifanya vazi LA taifa hakika watu wataona ni njia ya kuislimisha njia taratiiibu. Rais kavaa Ili kuwasapoti katika kipindi cha Mfungo wa Ramadhan na IDD. Ndo maana hutakaa umuone Kiongozi wa Kiserikali yeyote kaenda kwenye shereheza kidini ya Kikristo akavaa kanzu na baragashia. Zanzibar wamelikubali kwa sababu zaidi ya asilimia 95 ni waislamu.

Kwanza Mh Nape Nnauye Waziri wa Utamaduni,Michezo na Habari,alishafunga mjadala wa kulitafuta vazi la kitaifa. Linaonekana kuwa mgumu na usioleta majibu ya kuridhisha.
 
Mkuu unaweza kuwa sahihi lakini mimi naona vazi zuri la taifa ni uadilifu na uzalendo vazi linaweza kuwa kama kumvika chui ngozi ya kondoo.
Tumeona mazazi mengi lakini hayajabadili tabia za watu.
Badala ya kufikiri mavazi tufikirie njia ya kujenga uzalendo na uadilifu kuanzia chekechea.
 
Kwanza Kanzu na Baragashia linavaliwa Sana na Waislamu
Wacha kasumba za kikoloni, nchi yetu haina dini. Kanzu na kofia ya kiua (baraghashia)sio tu vazi la heshima kama lilvyo vazi la Nigeria lakini linampendezesha mtu na linaafiki hali ya hewa ya nchi yetu kwa ujumla. Ni vazi la Taifa la Zanzibar na si la kidini. Masheikh na maimamu hawavai koti, kanzu au baraghashia wakati wa kuongoza ibada ya waislamu. Muangalie Mufti alievalia kiislamu, ana kashda begani na kilemba! Usichanganye mambo.
7.jpg
 
Huo ndo ukweli. Kubali ukatae. Kwanza unajisumbua bure kwa sababu huo mchakato ushapigwa chini na Waziri husika. Halitekelezeki na wala halitimiziki. Asante kwa maoni yako lakini pole hayana manufaa kwa sasa.
 
Back
Top Bottom