Wakati wa mabadiliko umewadia

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Kuna kitu najaribu kuandika lakini mpaka sasa sijajua kitaitwaje ndio nimeanza tu usiku wa leo , nimekaa tu nikaona nianze kuandika mfululizi wa kitu Fulani ambacho sijui kitaishia wapi hata hivyo naomba mungu nizidi kupata nguvu na ujasiri wa kuendeleze hichi nilichoanza ili kiweze kuja kuwa kitabu kamili .

Najua sasa mimi na wewe tumechoka na hali ya kisiasa nchini mwetu pamoja na ya kiuchumi, ndio taifa letu lipo kwenye hatua mbaya sana mpaka sasa , tunaweza kuliokoa tu pale mimi na wewe tukiweza kuondoa tofauti zetu za kikabila , dini na kichama tuwe kitu kimoja tusimamie Utaifa wetu , Utaifa wetu ndio uwe kitu cha kwanza mengine yote yafuate nyuma , tuache dharau , kejeli na aina nyingine za maneno ya kukatishana tamaa .

Angalia sasa hali ya Taifa mabenki , na sekta ya fedha ilivyo katika dhiki ya hali ya juu viwanda vyetu navyo viko katika majonzi makubwa pamoja na wafanyakazi wake , wanafunzi wa vyuo wengi ambao hawana kazi na wanashindwa kujiajiri wenyewe , wasichana wetu wakisafirishwa kila siku kwenda katika nchi za watu kwa ajili ya biashara za uhahaba na kuuzwa , maisha yamekuwa gharama sana haswa mijini , riba kubwa , dhamani yetu ya hela mara kwa mara huwa inashuka dhamani , miundombinu iliyopitwa na wakati au iliyojengwa bila kufuata viwango vinavyotakiwa , wananchi waliokatishwa tamaa ambao kila siku wanajazana kwenye balozi za nje kutafuta visa ili wakatafute maisha mapya kwenye nchi hizo .

Ndugu jamaa na marafiki zangu wote nchi yetu inahitaji mabadiliko huu ni wakati wetu wa mabadiliko sisi vijana , ni wakati wa kubadili nchi hii na jamii yake kwa ujumla , ni wakati wa kuchagua serikali ambayo ina mipango inayoweza kutekelezeka , viongozi wanaosikiliza wananchi na kujadiliana nao mambo ambayo yana maslahi kwa wananchi hao kwa wakati huo hata miaka mingi ijayo , wale viongozi ambao wako madarakani kwa misingi ya kikabila na kidini au aina nyingine ya kutugawa bado wako madarakani na ndio hao walioipeleka nchi hii mpaka hapa ilipo .

Nchi yetu imekuwa inadidimizwa na kundi Fulani dogo la watu lilipo madarakani kwa msaada ya watumishi ambao hawana uzalendo na nchi hii hata kidogo lakini ni wajibu wa maadili yetu kuhakikisha nchi yetu inarudi katika wakati mzuri ambao baba wa taifa letu aliuacha pamoja na waasisi wengine wa taifa hili la Tanzania .

Historia inaonyesha vitu kama Ubaguzi wa Rangi maeneo kadhaa duniani haswa afrika , uonevu kwa wanyonge , ukoloni , utumwa na udikteta uliharibiwa au kufikishwa kikomo kutokana na nguvu za ummah , wacha tuweke rasilimali zetu pamoja chini ya mwovuli wa mabadiliko Tanzania , tubadilishe upepo wan chi yetu kwenda katika njia na mwelekeo mpya wa mabadiliko ya kiuchumi , kijamii na siasa .

Tunahitaji mabadiliko ya uongozi wa taifa hili na wote wa Afrika, na ili kufanikisha hili, tunahitaji mabadiliko ya jumla katika uendeshaji wa serikali na kuleta mageuzi ya kiutamaduni na kuondoa rushwa hizi na hivyo kuitwa viongozi wa Afrika. Kwa kuhimiza uhuru kwa wanaharakati wote Afrika kwa mara nyingine tena, kama harakati za uhuru wa Afrika na ukombozi kutoka ukoloni.

ITAENDELEA WAKATI UJAO
 
Back
Top Bottom