Wakati wa kusubiri unafanya nini?

hyassin92

JF-Expert Member
Oct 4, 2017
583
631
*WAKATI WA KUSUBIRI UNAFANYA NINI?*

Makala ya tarehe 3/4/2017(miaka 2 iliyopita)

Maisha yetu yamejawa na Hali ya kusubiri.Kusubiri maana yake ni kungojea. Ulipomaliza darasa la saba ulisubiri matokeo, mama anapobeba mimba anasubiri mtoto, ulipoomba kazi ulisubiri majibu, unapopata kazi unasubiri kustaafu.

Unaweza sasa kuona kuwa maisha yetu hapa duniani ni kusubiri tu. Kuna watu mpaka Leo kwa Wale waajiriwa wanasubiri mshahara wa mwezi wa tatu.

*SWALI Langu ni Je, tunafanya nini wakati wa kusubiri??? Pengine hili ndilo Swali la muhimu kujiuliza*

_Siku Moja nikiwa kwenye gari tulikutana na foleni kubwa sana eneo la Tazara .Foleni ilikuwa kubwa sana na sasa tukawa Tunasubiri taa au askari aturuhusu nasi tupite. Wakati tukisubiri abiria walianza *kulalamika* Huku wasijue Kwanini magari ya upande wetu yalikuwa hayaruhusiwi kumbe mbele Kulikuwa na ajari na hivyo tusingeweza kupita_

*Wakati wa kusubiri si wakati wa kulalamika*

Unapokuwa ukisubiri jambo si vizuri kuanza kulalamika kwa kuwa Hujui Kwanini linachelewa. Kila jambo hutokea kwa sababu Fulani.Kila jambo Lina majira na wakati wake. Unaweza kudhani kwa Akili yako kuwa linachelewa kumbe wakati wake bado. Huwezi kulazimisha mahindi yakomae kesho wakati umeyapanda Leo.

Kuna wakati unasubiri biashara yako ianze kuleta Faida lakini kila siku unaona hasara. Wakati Kama huu Ni Mgumu Sana kibinadamu na watu wengi Huwa wakifika hatua hii huamua kabisa kuachana na biashara na kumbe ulikuwa wakati wa kusubiri na kuona namna biashara inavyoweza kuanza kuleta Faida pengine kwa kubadili mbinu za Kibiashara.

*Wakati wa kusubiri ni wakati wa kujiandaa*

Wakati wa kusubiri si wa kukaa tu Huku ukisubiri jambo fulani kutokea bila kuwa na maandalizi .Mama mjamzito anapokuwa akisubiri kupata mtoto Huwa na maandalizi ya kumpata mtoto. Maandalizi ya mama ni pamoja na kufanya Mazoezi, kula chakula kizuri, kwenda kliniki n. K.

Nimekutana na wasomi wengi ambao wakati wakisubiri serikali iwaajiri wao wanakaa tu kusubiri waitwe kazini waanze kazi. Hawajiandai kwa lolote hata kupata maarifa ya kuwasaidia kufanya kazi kwa ufanisi na kwa ubora. Hawatafuti hata mahali pa kuanzia hata kama ni padogo mwisho wanaishia kulalamika.

*Wakati wa kusubiri ni wakati wa Kujaribu vitu vingi*

Kama unasubiri kuwa mtu fulani baadae ni muhimu wakati ukisubiri ukaaanza Kujaribu vitu vingi hata kama nashindwa Mara nyingi. unapojaribu Unajifunza na kupata uzoefu wa maisha.

Acha kukaa tu ukisubiri muujiza bila kujaribu chochote katika maisha yako.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom