Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 125,742
- 239,381
Baada ya TBC kwa kushirikiana na Nape Nnauye kuhakikisha vikao vya bunge vinakuwa siri mithili ya operesheni ya Mama Mzazi kwenye chumba cha upasuaji , umefika wakati wa kuwaonyesha watanzania kile kinachoendelea ndani ya bunge .
Upo umuhimu mkubwa sana kwa wenye nchi yao kufahamu hatua kwa hatua maswali yanayoulizwa na hoja mbalimbali zinazojadiliwa na kuwaona kwa macho yao waheshimiwa wabunge waliowachagua ili kujiridhisha na utendaji wao .
Kwa mfano mimi erythrocyte nimewafahamu wabunge wengi sana , vioja na vituko vyao kwa kuangalia matangazo ya bunge yaliyokuwa yakirushwa moja kwa moja .
Niliwafahamu wabunge ambao ni maarufu kwa kugonga meza , nimewajua wabunge na mawaziri ambao ni wasinziaji , kubwa zaidi nimewafahamu wabunge wenye hoja makini na watetezi wa kweli wa maendeleo ya wananchi na waliojitolea kwa kiwango cha juu kabisa kulinda rasilimali za taifa .
Ni muhimu sana kwa forum hii inayosomwa na watu wengi zaidi kuchukua jukumu hili kwa njia halali ama kwa njia za panya kama zitumikazo kwenye mambo mengine ya kufichua uozo na kunusuru taifa letu .