Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 13,610
- 21,186
Ni ukweli usiopingika kuwa raia wa Tanzania ni mchanganyiko wa raia kutoka mabara tofauti; Asia, Ulaya, Amerika na Australia. Bendera ya Taifa kama nembo ya Taifa inapaswa kuwakilisha raia wake wote bila ubaguzi. Kwa kuwa rangi nyeusi katika bendera ya Taifa inawakilisha waafrika weusi ni dhahiri haiwatendei haki raia wenye asili ya mataifa mengine.
Hivyo wakati umefika kubadilisha bendera ya Taifa kwa kuiondoa rangi nyeusi ili kutowakwaza raia wenye asili ya mataifa mengine. Kwa kufanya hivyo tutaimarisha umoja na mshikamano kama Taifa moja bila chembechembe yo yote ya ubaguzi wa rangi!