Mgambilwa ni mntu
JF-Expert Member
- May 30, 2017
- 2,869
- 3,188
Ulimwengu Ujulikanao (Observable Universe) unapanuka (expand) kwa kasi kubwa sana ya km 73.8 kwa sekunde (kwa megaparsec 1) na kwamba kadri Galaxy inavyokuwa mbali na Milky Way, ndivyo kasi ya kuexpand inavyoongezeka zaidi, hivyo Galaxy iliyo kwenye megaparsec 2 inapanuka kwa kasi kwa mara mbili zaidi (km 147.6 kwa sekunde). Hivyo, mwanga ambao unatoka kwa sasa kwenye galaxies za mbali sana, hautaweza tena kuifikia Dunia kwani galaxies (Nyota) zilizotoa mwanga huo zinazidi kwenda mbali na Milky Way Galaxy (liko Dunia). Kwa hali hiyo, hatutaweza tena kujua vitu vyovyote vinavyofanyika maeneo ya mbali sana ya Universe (mf. yaliyo miaka bilioni 40 ya mwanga). In fact, hata vitu vilivyofanyika miaka milioni 1 (hata bilioni 1) iliyopita kwenye eneo lililoko 40 billion light years, bado mwanga wake haujafika duniani. So, nini kimefanyika katikati hapo?
Hali hii imesababisha baadhi ya Wanajimu kudai kuwa, kuna uwezekano mkubwa wa uwepo wa Universes nyingine ambazo ziko mbali na Ulimwengu (Observable Universe) tuishimo na hivyo mwanga wake bado haujafika na kamwe haitatokea tena mwanga huo ukafika duniani kwa kuwa ziko mbali mno.
Eneo lililozungushiwa kibox cha njano ndilo pekee kwenye Galaxy ya Milky Way linaloonekana wakati wa usiku kutokea duniani.
Aidha, Ulimwengu Ujulikanao (Observable Universe) unaundwa na vitu vingi vikiwemo: nyota, sayari, vimondo, mavumbi (dust particles), dark matter, dark energy, dark radiation, black holes, white holes, etc, etc.
Kulingana na makadirio ya Ulimwengu Ujulikanao (Observable Universe), kuna:
- Galaxies zipatazo bilioni 200 - trilioni 2;
- Nyota zipatazo bilioni 100 kwenye Galaxy ya Milky Way pekee (Zidisha na Galaxies?); na
- Sayari zipatazo bilioni 1 kwenye Galaxy ya Milky Way pekee (zidisha na Galaxies), huku zaidi ya Sayari milioni 500 kwenye Milky Way zikiwa na mazingira yanayoweza ku-support life.
Kitabu cha Ufunuo kimeweka hesabu za malaika kuwa zaidi ya malaika milioni 100.
Kwa upande wa Dini ya Kihindu, wao wana miungu (devatas na devees) ipatayo 333,333,333. Ukiwachukulia hao kuwa ndio fallen angels, basi malaika waliobaki mbinguni wakimtii Mungu (2/3) ni 666,666,666. Ukijumlisha na Shetani (Devil) unapata jumla ya malaika bilioni 1.
Wengine wamekuwa wanalinganisha idadi ya malaika na wingi wa nyota ulimwenguni. Kwa kuwa kuna matrilioni na matrilioni ya nyota, basi wanaamini kuwa, hizo nyota ndio hao malaika.
Swali: Ilikuwaje Wanadamu wawili tu (Adam & Eve) ndio waumbwe na kuwekwa kwenye Galaxy ya kawaida sana "Milky Way" kati ya mabilioni ya Galaxies? Ilikuwaje pia hao wanadamu wawili wawekwe wenyewe tu kwenye Sayari ya Dunia miongoni mwa mabilioni ya Sayari zilizoko kwenye Milky Way Galaxy?
Hayo matrilioni na matrilioni ya sayari ulimwenguni yana kazi gani?
Je, kuna akina nani wanazifaidi hizo Sayari zilizozagaa ulimwengu mzima?
Huko kwenye Unobservable Universe kuna nini?
Je, si kweli kuwa kuna Universes nyingine nyingi zaidi ya hii tuliyomo?