Wakati Tuajitahidi Kutafuta Ukombozi wa Taifa. Tusisahau Ukombozi Binafsi

Kaldinali

JF-Expert Member
May 25, 2012
263
138
Wakuu

Kuna suala la muhimu ambalo ningependa tujikumbushe na kulizingatia. Wakati tunashirikiana na kufanya kazi kwa pamoja kujaribu kuondokana na uozo wa chama cha mapinduzi ili kuikomboa nchi yetu, ni muhimu juhudi hizo ziende sambamba na jitihada za kujikomboa kibinafi. Nnapoongelea ukombozi binafsi nna maanisha ni muhimu kujiandaa vizuri kwaajili ya ushindani binafsi unaoendelea katika jamii. Katika vyama tutapa ukombozi wa kitaifa. Ila wakati huo huo kila mtu binafsi anapaswa kufanya kazi kwa bidii kujiandaa au kujiendeleza yeye binafsi na familia yake.

Kama wewe ni mtu mwenye miaka kati ya 30 mpaka 45 na haujasoma na kuwa na degree na diploma utakuwa unakosea. Binadamu tumepewa nafasi ya kuishi duniani mara moja tu. Swali ni jeje wewe unataka kuishi maisha ya aina gain katika jamii. Jamii yetu imegawanyika kati ya walionacho na wasionacho na kwakiasi kikubwa tufauti yao imeletwa na ELIMU. Asilimia kubwa ya walionacho ni watu waliosoma vizuri na kupata kazi inayoyawezesha kumudu maisha, kuwa na hakiba, kuwa na vitega uchumi na hatimae kuwa na utajiri. Kama na wewe umechagua kuishi maisha mazuri katika miaka yako hii michache hapa duniani (your only one life) ni lazima usome vizuri ili uweze kuvuka kutoka katika tabaka la wasionacho na kwenda kwenye tabaka la walionacho. Kuna njia nyingi ya kuweza kuvuka daraja hilo ila njia ya uhakika kuliko zote ni ELIMU.

Mimi nilipata bahati ya kwenda kusoma Marekani. Kuna jamaa kama 6 walinipokea na tukaishi wote vizuri sana. Nilipomaliza masomo nikarudi nyumbani nikapata kazi na sasa nnaendelea vizuri sana na maisha. Jamaa wawili kati ya wale 6 walionipokea walirudishwa Tanzania. Kwa bahati mbaya hawa jamaa hawakusoma kule marekani. Tulipokuwa kule tulikuwa na maisha sawa tu kwakuwa kule kila mtu anaweza kupata kazi kirahisi. Sasa wamerudishwa nyumbani hawa mabwana wanahangaika sana. Hawana kazi na hawawezi kupata kazi. Hawakujiwekewekea akiba hivyo hawawezi kuwa wafanyabiashara. Inatia huruma watu wazima kama hawa kurudi na kuja kuishi kwa wazazi wao kama jobless. Wakati tunashirikiana na kufanya kazi kwa pamoja kujaribu kuondokana na uozo wa chama cha mapinduzi ili kuikomboa nchi yetu, ni muhimu juhudi hizo ziende sambamba na jitihada za kujikomboa kibinafi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom