Wakati polisi wanatangaza kuua washukiwa,vyombo vya habari navyo vinatangaza washukiwa wanaua tu

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
Anaaandika Dotto Bulendo.
Kindercrazy

1.Wakati polisi wanatangaza kuuwa washukiwa,vyombo vya habari navyo vinatangaza washukiwa wanaua tu.Kindercrazy

2.Wakati watuhumiwa wakuu wa Escrow wakiwa Rumande,mmoja wa waliopata mgao anatangaza hadharani kuwa ni kweli alipokea,anaamua kuzirejesha serikalini.Kindercrazy.

3.Mwaka 2015,serikali walikuwa wakali kwa yeyote aliyesema pesa za Escrow ni za umma,mpaka Mh Rais mstaafu Kikwete aliauambia umma kuwa hizo zilikuwa si pesa za umma,waliosema ni za umma waliitwa tumbili,leo mtuhumiwa wa mgao anapeleka serikalini pesa zilizoitwa na mtu binafsi,sasa sijui ndiyo mwisho hapa?kindercrazy.

4.Sheria ya kutakatisha pesa inasema mtu yeyote ambaye alijipatia ama amejipatia pesa kwa njia haramu na kuziingiza kwenye shughuli halali,atashtakiwa chini ya sheria hii,kwenye huli la Escrow,baadhi wapo Rumande,wengine wamerudisha,wengine hawajarudisha na wapo mtaani tu.kindercrazy.

5.Polisi wanatangaza kuua watuhumiwa wa mauaji huko Pwani,baadhi ya magazeti yanaandika,"Polisi waua"mengine yanaandika,"Polisi yadai kuua".kindercrazy.

6.Vichwa vya treni vinakuja mpaka bandari ya Dsm,vina label ya TRL,Rais anakwenda bandarini anawauliza TRA,TPA,TRL kuwa ni vya nani?wote wanasema hawajui,baadae wanamtandao wanavujisha taarifa kwa vyombo vya habari pmj na video clip inayoongelea vichwa vya treni lakini bado haijulikani ni vya nani?!!.kindercrazy.

7.Hivi ndani ya jamii,polisi na mahakamani ni kwa ajili ya nani?Kindercrazy.
 
Singeri, taarabu, mnanda, mdundiko,segere, mganda,zote ngoma zetu...
 
Hiyo namba 7 polisi na mahakama ni kwaajili ya WAPINZANI
 
Sasa unacho shaangaa mleta mada ni kitugani? Polisi wapo ili kulinda usalama waa watu na malizao, wanaweza kutumia nguvu kubwa, nguvu kiasi, au kwa ushawishi Ila ayo yote itategemea na aina ya uhalifu wanao pambana nao.

Swala la uhalifu/mauaji nivitu ambavyo vipo sio hapa tu kwetu. Duniani kuanzia Afrika, America , Ulaya ayo makundi kama ya kibiti yapo.

Kinacho fanyika na Polisi ni kutumia ujuzi na mbinuzao zote kuyamaliza, ila itachukua muda kuyadhibiti. Kwaiyo vifo kutokea nijambo ambalo unatakiwa ufahamu litakuwepo.Hii inatokana na aina Yenyewe ya wahalifu. Tunachotakiwa kufanya ni kuliunga mkono jeshi la polisi kwa kujaribu kutoa ushauri, nini kifanyike n.k

Wenzetu uko nje wananchi wanashirikiana na polisi ili kumaliza uhalifu, kwakua wahalifu tunaishi nao majumbani kwetu. sio kutoa maneno ya kuudhi na kukatisha tamaa jeshi hilo.

Sent from my TECNO W4 using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom