S.N.Jilala
JF-Expert Member
- Jan 26, 2012
- 540
- 507
Wakati Mwingine unatamani kusikia Magazeti yetu yakiwa na vichwa vya habari zifuatazo.
1. Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam College ya Injinia wamefanikiwa kutengeneza daraja wakiwa wanafanya majaribio na daraja hilo litakaa miaka 50 ndiyo liweze kuhitajika kufanyiwa marekebisho. Ni daraja la kisasa kabisa kutokea.
2. Chuo cha Taifa cha Usafirishaji kitazindua helkopita mpya na ya kisasa kabisa mwezi huu ambayo imetengenezwa na wanafunzi wa chuo hicho na Rais ataenda kuizundua helkopita hiyo mwezi ujao.
3. Tanzania imeimarisha zaidi viwanda vyake ambayo ni nguzo ya viwanda vyote nchini. Viwanda hivyo viko chini ya Serikali ya Tanzania ambavyo ni vya Chuma, Kemikali na Injinia.
4. Tanzania inaweza kuwekewa vikwazo vya uchumi kwa kusisitiza kuwa viwanda vyake vya nyuklia ni kwa sababu ya nishati ya umeme tu na si vingine.
5. Msanii tajiri kuliko wote Afrika kutoka nchini Tanzania atafanya ziara kubwa nchini Marekani na Wasanii wa Marekani wanapigana kumbo ili angalau kumuomba wamshirikishe kwenye nyimbo zao.
6. Tanzania ndiyo nchi inayoongoza kwa kuwa na uchumi imara Afrika.
8. Tanzania ni nchi pekee Afrika ambayo kila Mtanzania ana uhakika wa kupata maji na umeme kwa kiwango cha asilimia themanini mijini na vijijini.
9. Rais wa Tanzania kesho atasafiri kwenda Mbeya na baadaye ataenda Kigoma kwa kutumia treni ya mwendo kasi.
10. Wakulima na Wafugaji nchini Tanzania hali zao kiuchumi ni imara zaidi kwa sababu serikali inawajali na kuwawezesha sana.
11. Madaktari kutoka Tanzania wamegundua dawa ya kuzuia kansa na ukimwi.
12. Rais wa Tanzania apewa zawadi ya Mo Ibrahim kuhusu utawala bora baada ya kukosa mshindi miaka mingi.
Natamani Magazeti yetu siku moja yaandike hivyo. Ni lini?. Sijui, lakini kwa Mwenyezi Mungu yote yawezekana. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.
02/03/2017.