Wakati mwingine ni bora kutokujua

Gurta

JF-Expert Member
Sep 17, 2010
2,234
531
Kwa walikuwa wanatazama 'Kipima Joto' ITV watakuwa wamemuona mzee mmoja hivi anasema yeye ni mstaafu.

Nikiangalia na kutafakari zile takwimu alizokuwa nazo na kuzi-present pale, naona napata hasira zaidi tu. Natamani tu kama nisingeyejua haya. All that kodi that is not collected, inefficiency, thousand ignoramuses making policies for this country, the free electricity and telephone unit for our blessed wakubwa! Basi tu

Haya mambo mengine.....
 
ni kweli maana kwa jinsi mifumo ya nchi yetu ilivyo hata ukijua huna cha kufanya kutokana na kulindana kulikokithiri
 
Wakati mwingine ni afadhali usijue ili upate faraja ya muda kisha uje ujute pale ambapo tatizo kubwa litakuja kutokea ghafla. Mimi napenda watu wajue madudu yanayofanywa na wateule wetu, "waliojaliwa kula mema ya nchi" ili tuweze kuzinduka na kujua kuwa hawa watu sio wenzetu. Inatia kinyaa kuona watu wanashabikia watu wachafu wasioitakia mema nchi hii kwa ujira wa pilau na kupandishwa vyeo pindi wakubwa wakipata madaraka...shame on us!

Waache watu wenye data wazitoe ili watz wengi waweze kufunguka kutoka kwenye mawazo mgando.
 
Back
Top Bottom