Wakati muda ungalipo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakati muda ungalipo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Graph Theory, Sep 17, 2012.

 1. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #1
  Sep 17, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,804
  Likes Received: 1,118
  Trophy Points: 280
  Walioishi kabla yetu walipata kunena hivi Mwenzako akinyolewa, zako tia maji. Mwalimu mzuri kuliko wote ni jamii maana namna watu ndani ya jamii wanapopambana na matatizo mbalimbali ni somo tosha kwa yule ambaye kwa wakati huo hapambani na tatizo hilo, na siku likimpata atakuwa ameshapata mbinu nzuri za kukabiliana nalo. Na jambo ambalo vijana tunatakiwa kujiandaa kwalo ni suala la ndoa. Katika kujifunza kwangu kwa jamii ya watu ambao wameshaingia ndani ya ndoa nimejifunza yafuatayo ambayo nimeona si vyema kukaa nayo moyoni peke yangu na hivyo nimeamua kuwashirikisha.

  JAMBO LA
  KWANZA


  Hakikisha kuwa unafuatilia tabia za wazazi wa yule unayetaka kuoana naye. Na hii ni kwa sababu enzi za uchumba, kila mmoja huwa anajitahidi kuficha tabia zake halisi lakini ni rahisi kungundua tabia alizonazo kupitia kuangalia maisha ya wazazi wake. Na nikwakuwa mtoto mara nyingi anaiga tabia za wazazi toka akingali mdogo. Na pia tabia za wazazi ndizo zitaongoza katika malezi ya mtoto wao. Hauwezi ukakuta mzazi ni mcha Mungu halafu walee mtoto wao nje ya maadili ya Mungu, au wazazi si wacha Mungu halafu walee mtoto katika misingi ya KiMungu.

  JAMBO LA
  PILI


  Katika kufuatilia kwangu ni ndoa za watu gani ambazo zinadumu, nikapata jambo hili. Ndoa nyingi ambazo mme ana herufi ya mbele kuliko herufi ya kwanza katika jina la mke, ndoa ya namna hiyo inadumu kuliko ile ambayo mke ndiye ana herufi ya mwanzo katika mfumo wa alphabeti kuliko mme. Kwa kuwa majina yah wanandoa ambao nimefanya utafiti huu kwao hamuwajui naomba nitumie mifano ya ndoa zilizoandikwa ndani ya Biblia takatifu maana angalau hao watakuwa wanafahamika kwa wengi.
  Adamu na Eva, ukiangalia haya majina herufi ya kwanza katika jina la Mme inatangulia ile ya mwanamke, na hakuna sehemu ambayo tunasoma kuwa hii ndoa ilivunjika.
  Ndoa ya pili ni ya Ibrahimu na Sarah, licha ya ndoa hii kumaliza muda mrefu pasipo kuwa na mtoto lakini bado ilidumu.
  Ndoa nyingine ambazo mwanamme alikuwa na herufi inayotangulia herufi ya kwanza katika jina la mkewe na ndoa zikadumu ni kama ifuatavyo. Ndoa kati ya Isaka na Rebeka, pia Elikana na Hana. Mifano ni mingi sana lakini kwa leo naomba niishie hapo.
  Nakaribisha mawazo pia kutoka kwenu maana ni lazima kuelezana ukweli wakati muda ukingalipo.
   
Loading...