Mkuu ni kwasababu zifuatazo..kwanini Waganda hawako bitter na jinsi jumuiya ilivyovunjika mwaka 1977 kulinganisha na sisi Watanzania?
..au kwanini Waganda hawana hofu na jumuiya mpya kulinganisha na Watanzania tunavyoiogopa jumuiya?
..kwanini Watanzania hatuko tayari ku-embrace / ku-dominate jumuiya mpya ya afrika mashariki wakati tulikuwa na miaka 43+ ya kujiandaa toka 1977 mpaka 2021?
Mkuu ilipoanza EAC ya leo mjadala ulikuwa kuhusu transition period...nadhani wakati umefika kwa Tz kuwa na MKAKATI wa muda mfupi, na muda mrefu, wa kuwaandaa vijana wetu kwa mabadiliko na fursa zinazojitokeza ktk Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Wakenya wanatutaniaga kwamba bado tuna hangover ya ujamaa. Kikweli siyo hangover bali bado tumelewa. Ujamaa ndiyo unafanya monopoly na protectionism kila sehemu. Monopoly hadi kwenye elimu. Kukiwa na monopoly ubunifu kunakuwa hakuna kabisa.Mkuu ilipoanza EAC ya leo mjadala ulikuwa kuhusu transition period.
Tanzania ilitaka miaka 10 na nakumbuka miaka ya Kikwete ilikusudiwa hivyo.
Haraka haraka za CoW (Coalition of Willing) zililete mzozo na hoja kubwa ya Tz ilikuwa muda wa kujiandaa. Ni miaka 15 tangu JK aondoke na zaidi ya 23 ya EAC mpya, bado hatujajiandaa!
Kwa muda mfupi, soko liwe huru hasa la ajira. Vijana wetu watajifunza ushindani na si kulindwa na monopoly zilizojengwa juu ya sheria.
Kwa muda mrefu,lazima mitaala ya elimu iangaliwe, ijengwe katika uhalisia wa mazingira na si kukariri.
Maeneo ya taaluma yawe huru ili kuibua chem chem za fikra, kupambanisha hoja, kuchambua na kuchambuliwa.
Ndivyo Makerere na Nairobi wanavyofanya na hilo linawajengea sana vijana uwezo wa kutafiti, kujieleza na kutetea hoja kwa mantiki.
Utakumbuka zama UDSM kulikuwa na mijadala kila kona ya namna mbali mbali, iwe sheria, uchumi, siasa n.k
Palipokuwa na mjadala pale Nkrumah wanafunzi wa vyuo jirani walihudhuria
Wageni kama Marais walialikwa UDSM
Leo hali ipoje? ni kama highschool kubwa tu kwasababu uhuru wa taaluma ''academic freedom' haupo.
Katika soko la utandawazi ''globalization'' dunia haitafuti mabingwa wa kukariri, inatafuta watu wanaofikiri, kuyaona matatizo, kuyaeleza na kutafuta ufumbuzi. Swali, vijana wetu nafasi yao ipo wapi?
Kama kuna mambo yanayokera ni kusikia eti kuna Wakenya/Waganda wamenyimwa vibali vya kazi Tanzania.
Mashirika na Kampuni za dunia zinatafuta 'waajiriwa local' ili kupunguza gharama, lakini zinachukua wa nje
Swali, ni kwanini organization zimekubali kuchukua gharama hizo?
Pengine jibu ni rahisi kwamba ukipata qualified person mwenye mtazamo mpana ni bora kuliko kijana wa Tanzania atakayeajiriwa bila tija katika organization husika.
Solution si kuwanyima vibali, bali kuwaachai watoe changamoto kwa vijana wenyewe wakisema '' watatia akili''.
Bila hivyo huu mwendo wa mbeleko unazidi kuwadumaza tu!
Matokeo yake ni kutaka protection kila siku badala ya kufikiri namna ya kupambana.
Baada ya EAC kuvunjika nchi wanachama zilimteua, Dr.Victor Umbricht, raia wa Uswizi, kuwa msuluhishi wa kugawa mali na madeni ya jumuiya.
Kwa msingi huo, siyo sahihi kusema kwa nchi fulani ilidhulumiwa, au kuwa na chuki na nchi fulani kwamba imeiba mali za jumuiya.
Kwa upande mwingine, serikali ya Tanzania ilipewa fedha za pensheni za watumishi waliokuwa wakifanya kazi ktk taasisi mbalimbali za jumuiya. kwa bahati mbaya serikali ilizipangia fedha hizo matumizi mengine na kusababisha malalamiko na mgogoro mkubwa wa "wastaafu wa jumuiya ya afrika mashariki."
cc Nguruvi3, Mohamed Said
Walishauma mashukaNa wale wazee mpaka wamekufa wamedhulumiwa hela zako
Nakumbuka kuna kipind walikua wanaandamana sana hapo mjini enzi za Gewe/Tibaigana.
Saivi naona walishakata tamaa
Amini aliingia 1971 nadhani umeteleza kidogoKuna makosa fulani katika mahojiano hayo, ndiyo maana mahojiano hayo yanabidi yachukuliwe kwa context ya hali halisi iliyokuwapo siyo kwa maneno ya mahojiano. Kwa mfano Umbritch ameweka tamko la Obote mwaka 1977 na waganda kukikimbia nchi lakini Amin alipokuja madarakani mwaka 1977 bado hawakurudi; unaona wazi kabisa kuwa statement hiyo haina ukweli ingawa maana yake ni sahihi.
Kusingetokea vita ya Uganda, ripoti ile isingekubaliwa kabisa, kwa hiyo Kenya walikua na opportunity kubwa sana kwa ya report hiyo kutolewa at the right time! Jambo lililosababisha KQ kunyanuka mara moja!
Hukuelewa nilchoandika; sikuandika kuwa Amin aliingia madarakani mwaka 1977!Amini aliingia 1971 nadhani umeteleza kidogo