Nimesoma haya mahojiano yote, yanafungua macho. Shukrani kwa kuyaweka hapa.Ule mgawanyo wa Umbritch haukuwa fair, ila nchi zililazamika kukubaliana ili mambo yaishe hasa kwa vile wakati huo Tanzania na Uganda zilikuwa zimetoka vitani; alifanya kazi ya usuluhishi kwa karibu miaka kumi akamaliza mwaka 1982 baada ya vita. Ukisoma mahojiano yake hapa kwenye ukurasa wa 10 utaona kuwa hakukuwa na consensus kabisa kuhusu mgawanyo huo ambapo Kenya ilipata zaidi ya Tanzania wakati Uganda ndiyo iliyoonewa zaidi. Anasema mgawanyo wake ulifuata indicators za IMF, ambazo wakati huo zilikuwa zinaipendelea sana Kenya politically wakati huo kwa kuwa na uchumi ambao ni "market oriented"..
Nashukuru sana mkuu
Ila kutokana na hoja hii, ilitakiwa kwenye Mkataba wa EAC2 wa 1999; Kenya ichangie zaidi kwa kuwa ilifaidika zaidi na anguko la EAC1
Kwa nini wachumi hawakulirudisha hili mezani
Kichuguu,
Kwanza, nikushukuru sana sana kwa kutuletea document yenye mahojiano ya Dr.Victor Umbricht. kwa kweli umeutendea HISANI kubwa mjadala wetu, na wachangiaji wake.
Pili, bila waTz kuandika kwamba hawakukubaliana na mapendekezo ya Dr.Umbricht, na kubainisha ni vipengele gani hawakukubaliana navyo, basi maelezo ya msuluhishi yatabaki kuwa ndio ukweli wenyewe.
Tatu, kuna mahali Dr.Umbricht anasema Uganda / Obote alipinga baadhi ya mapendekezo yake, lakini mapendekezo hayo yalipohakikiwa tofauti ya alichopendekeza msuluhishi na walichopendekeza independent experts kilikuwa ni asilimia 1 %. kwa hiyo binafsi nalazimika kuamini kwamba Dr.Umbricht alifanya kazi yake bila upendeleo.
Hawakutumia kigezo cha IMF indicators, lakini mgawanyo wenyewe ulifanyika hivyo, kwani baada ya kuamaua kutumia geographical location na equality bado walikuwa wamo kwenye zile IFM indicators tuNimesoma haya mahojiano yote, yanafungua macho. Shukrani kwa kuyaweka hapa.
Huyu doctor anasema hicho kigezo cha kutumia indicator za IMF nchi zilikipinga hivuo hawakukitumia. Bali walitumia sababu za kijiografia na kuangalia usawa. Pia waligawana madeni ya jumuiya ambapo anasema nchi zilikuwa zinalipa vizuri sana.
Anasema nchi zilizopata assets nyingi zilitakiwa kulipa zile zilizopata assets chache ili kufikia usawa. Naona kama jamaa alifanya kazi nzuri sana. Na ndiyo umefanya hata huu ushirikiano wa sasa uweze kuwepo. Sioni kama kuna mtu alionewa.
Hili jumuia ilikuwa kubwa sana. Wafanyakazi 100,000 siyo mchezo!
Mkuu mashirika mengi yalikufa kwasababu ya kuendeshwa kisiasa zaid ya kiuchumi. Unakumbuka mwenyekiti wa tawi la chama katika shirika fulani alikuwa na nguvu kuliko meneja. Vyama vya wafanyakazi vikawa matawi ya chama tawala. Hakuna aliyeeleza ubovu au kuwasemea wafanyakazi.Shirika kama NMC liliendeshwa vibaya na lilipokuja kubinafsishwa lilikuwa hoi bin taabani. Mamlaka za mazao mbalimbali nazo hazikuwa na ufanisi kama ule wa vyama vya ushirika.
Azimio la Arusha liliharibu sehemu kubwa sana ya Uchumi wa nchi.Azimio la Arusha lilikuwa baya sana kwa upande wa uchumi. Uzuri wa azimio upo ktk masuala ya maadili ya viongozi.
Kuna point hapa. Dr Umbricht alisimamia mali na madeni (assets and liabilities of the defunct EAC)..Dr.Umbricht anasema timu yake ilitafuta mali / assets zote za zilizokuwa taasisi za East African Community na kuzigawa kwa namna ambayo nchi zote ziliridhika. Anasema alitafuta siyo mali kubwa-kubwa kama ndege, na mabehewa ya treni, bali alitafuta na kuhakiki mpaka mali ndogo kama typewriter!!
Hapa kuna mambo mawili unatakiwa kuyaangalia.Ila kutokana na hoja hii, ilitakiwa kwenye Mkataba wa EAC2 wa 1999; Kenya ichangie zaidi kwa kuwa ilifaidika zaidi na anguko la EAC1. Kwa nini wachumi hawakulirudisha hili mezani
Thanks BroNguruvi3,
..naomba hapo ulipomjibu Sita Sita uongezee kwamba nchi zote zilikuwa na mchango ktk kuanguka kwa EAC.
..Tanzania tulikuwa tunafuata mlengo wa KIJAMAA ambao hauendani vizuri na siasa za wenzetu wa Kenya.
..Kenya walikuwa ni MABEPARI ambao walikuwa wanatishiwa na ujamaa wa Tanzania.
..Uganda walikuwa wanatawaliwa na DIKTETA asiyetabirika na aliyekuwa na mgogoro wa kisiasa na majirani zake.
..Kuna taarifa kwamba ilifika mahali viongozi wakuu, yaani Kenyatta, Nyerere, na Iddi Amini, walikuwa hawawezi kukaa meza moja, kujadili, na kuamua masuala ya EAC.
..Tusiwalaumu Wakenya peke yao kwamba ndio waliovunja jumuiya. Kama Wakenya na Charles Njonjo ndiyo waliofitini jumuiya, mbona Tanzania na Uganda hazikuendeleza mashirikiano na kuunda jumuiya / coalition ya nchi mbili [ Tz & Ug ]?
Kuna makosa fulani katika mahojiano hayo, ndiyo maana mahojiano hayo yanabidi yachukuliwe kwa context ya hali halisi iliyokuwapo siyo kwa maneno ya mahojiano. Kwa mfano Umbritch ameweka tamko la Obote mwaka 1977 na waganda kukikimbia nchi lakini Amin alipokuja madarakani mwaka 1977 bado hawakurudi; unaona wazi kabisa kuwa statement hiyo haina ukweli ingawa maana yake ni sahihi.
Kusingetokea vita ya Uganda, ripoti ile isingekubaliwa kabisa, kwa hiyo Kenya walikua na opportunity kubwa sana kwa ya report hiyo kutolewa at the right time! Jambo lililosababisha KQ kunyanuka mara moja!
Nimewahi kukaa ofisi moja na mtu aliyekuwa mtaalam wa computer wa EAC huko Nairobi ambaye ni mtanzania,anasema wakenya walijiandaa kuvunja EAC kimya kimya, watumishi wa kitanzania na waganda walikuwa wanafichwa baadhi ya documents na kutengwa,ndege na treni nzuri zilipoingia Kenya hazikuruhusiwa kurudi Tz au Uganda, mpaka walipokamilisha walichokihitaji ndio wakatangaza hawahitaji tena EAC, japo mtu mmoja senior officer (kileo) wa Tz alitoa alert kwa Baba wa Taifa, labda ilisaidia kidogo...kulikuwa na crisis baada ya jumuiya kuvunjika, na ktk crisis hiyo ndiyo unasikia habari za rubani kutoroka na ndege. pia nimewahi kusikia habari ya mpaka wa Tz na Kny kufungwa, etc etc.
..lingine unalopaswa kukumbuka ni kwamba kila nchi mwanachama ilikuwa ina-host taasisi za Jumuiya kama vile bandari, reli, posta, shirika la ndege, pamoja na mali na miundombinu ya taasisi hizo. Kwa hiyo kila nchi ilirithi taasisi za jumuiya na kuzifanya za kitaifa.
vilevile kulikuwa na wafanyakazi wa Jumuiya. Wako waTz walikuwa wakifanya kazi Kenya, au Uganda, na pia walikuwepo raia toka nchi majirani waliokuwa wakifanya kazi Tz. kutokana hali hiyo ilibidi kila nchi ichukue raia wake na kuwarejesha nyumbani.
..Lakini baada ya hapo nchi wanachama zilimteua Dr.Victor Umbricht ambaye alifanya kazi kubwa ya kuhakikisha mali na madeni ya jumuiya yanagawanywa kwa haki. Binafsi sijasikia popote pale serikali yetu ikilalamikia utendaji na kazi iliyofanywa na Dr.Umbricht.
..Kuhusu nchi gani iliumia zaidi, nadhani ilitegemea nchi husika ilikuwa imara kiasi gani wakati wa kuanzishwa kwa jumuiya. Kama nchi A ilikuwa na uchumi mdogo kuliko nchi B wakati wa kuanzisha jumuiya basi hali ilikuwa hivyohivyo wakati jumuiya inavunjika.
Nasikia hii ilivunjika mwaka 1977. Nimekuwa nikisikia hadithi nyingi kuwa watu waligawana mali kama washenzi(barbarians). Hili limewapa baadhi ya watu vinyongo hadi leo kuwa walidhulumiwa, naomba kujua kwenye kugawana huko, Uganda alipata nini, Kenya alipata nini na Tanzania alipata nini?
Ndiyo makosa niliyosemaJamani mwaka 1977 nchi ya Uganda ilikuwa chini ya Idi Amini Dadaa, sasa Obote alipata wapi nafasi ya kuwa msemajia wa nchi ya Uganda Kumbuka Idi Amini aliongia madarakani mwaka 1971.
Jamaa hawa walitupigia mahesabu makali tukaingia mkenge. Ila maajabu ya Mussa, leo ndio wanapambana kweli kweli EAC irudishwe. A little too lateKenya ndyo ilipata vingi
Hili tatizo la kupangia pesa za watu matumizi mengine ni sugu sana.Baada ya EAC kuvunjika nchi wanachama zilimteua, Dr.Victor Umbricht, raia wa Uswizi, kuwa msuluhishi wa kugawa mali na madeni ya jumuiya.
Kwa msingi huo, siyo sahihi kusema kwa nchi fulani ilidhulumiwa, au kuwa na chuki na nchi fulani kwamba imeiba mali za jumuiya.
Kwa upande mwingine, serikali ya Tanzania ilipewa fedha za pensheni za watumishi waliokuwa wakifanya kazi ktk taasisi mbalimbali za jumuiya. kwa bahati mbaya serikali ilizipangia fedha hizo matumizi mengine na kusababisha malalamiko na mgogoro mkubwa wa "wastaafu wa jumuiya ya afrika mashariki."
cc Nguruvi3, Mohamed Said
Nimewahi kukaa ofisi moja na mtu aliyekuwa mtaalam wa computer wa EAC huko Nairobi ambaye ni mtanzania,anasema wakenya walijiandaa kuvunja EAC kimya kimya, watumishi wa kitanzania na waganda walikuwa wanafichwa baadhi ya documents na kutengwa,ndege na treni nzuri zilipoingia Kenya hazikuruhusiwa kurudi Tz au Uganda, mpaka walipokamilisha walichokihitaji ndio wakatangaza hawahitaji tena EAC, japo mtu mmoja senior officer (kileo) wa Tz alitoa alert kwa Baba wa Taifa, labda ilisaidia kidogo.
Huyo mfilisi alikuja kuwekwa miaka miwili baadae wakati hizo mali zote waliendelea kuzitumia smoothly as if EAC bado ipo ,wakati Tz na Uganda zikiumia kutafuta replacements ya zile zilizotoroshewa Kenya, Tanzania na Uganda ziliumia na hali hiyo. Sidhani kama utetezi wa maana sana, huyo rubani alisaidia kwa sababu inaonekana hiyo ndio ndege kubwa pekee tuliyoambulia.
Thanks Bro
Pamoja na kupigana na Uganda, Tanzania ilikua busy na ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika (Namibia, Angola, Zimbabwe, Afrika Kusini)
Resources nyingi zilipelekwa kuhudumia kambi za wapiganaji na familia zao
Kwa hiyo EAC ilionekana kama mzigo usio na manufaa kwa wananchi wa kawaida
kwa kuwa ilikua inanufaisha zaidi Kampuni kubwa zilizokuwa na uwezo wa kufanya cross border trade ambazo nyingi zilitokea Kenya na wamiliki wake ni Mabepari wenye asili ya nchi za Uingereza, Uholanzi na India.
Baada ya WW, Tanzania iliwekwa chini ya uangalizi wa Uingereza, Hawa jamaa kwa kuwa walikua na interests zaidi hapo Nairobi, walitugeuza sisi soko la bidhaa zao from Kenya. Mfumo wa kutegemea bidhaa za Kenya ulianzia hapa.
Hata ilivyokuja EAC ilijitahidi kupunguza utegemezi wa viwanda vya Kenya lakini bado haikuwezekana.
So far situation ipo hivyo hivyo, EAC inanufaisha zaidi Kampuni kubwa za Kenya
Unga wa Bhakressa unaletewa zengwe kuingia Kenya
Kioo Limited nao walipigwa kodi za ajabu ajabu wasiweze kuingia Kenya
Konyagi nao wanapigwa zengwe kila siku
Tutaendelea hivi mpaka siku tukiweza kuwafundisha watoto wetu umuhimu wa kutumia bidhaa za Tanzania.
Mkuu nakubaliana nawe 101%. Watanzania bado wanalalamika kuhusu resources zilizotumika katika ukombozi..Sisi Watanzania tunapenda sana kulalamika.
..EAC ya kwanza ilivunjika mwaka 1977.
..EAC mpya ilizaliwa mwaka 1999.
..Sasa tujiulize kwanini hatukujiimarisha ktk hiyo miaka 22 tuliyokuwa nje ya jumuiya?
..Halafu toka 1999 mpaka hivi tunavyozungumza ni miaka 20+ lakini bado Watanzania tuna malalamiko yaleyale kama ilivyokuwa mwaka 1977.
..Naipenda sana Tz na ninapenda tunufaike kutokana na mashirikiano na majirani zetu, lakini wakati mwingine nadhani Watanzania tunatumia muda mwingi kulalamika na hali hiyo inatuzuia kutafuta mbinu za kunufaika na fursa zilizoko ktk jumuiya.
cc Nguruvi3, Kichuguu