Junius
JF-Expert Member
- Mar 11, 2009
- 3,181
- 139
CHAMA cha wananchi (CUF) kimezindua mkakati mpya unaolenga kushinda uchaguzi mkuu ujao, huku ikitoa tuhuma dhidi ya serikali na Chama cha mapinduzi (CCM) kuhusu undanganyifu.
Katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliyofanyika katika viwanja vya Kibanda-maiti mjini hapa mwishoini mwa wiki iliyopita, viongozi wa chama hicho walizindua mkakati wa kuelekea Ikulu, na mkakati wa zinduka.
Katibu mkuu wa CUF maalim Seif Sharif Hamad, Naibu wake Juma Duni Haji, na Mkurugenzi wa uenezi Salum Bimani, kwa nyakati tofauti, waliwataka wafuasi wao kuunga mkono mikakati hiyo kwa kujinadkisha.
CCM chini ya Rais Kikwete, wamepanga mkakati wa kufanya uchaguzi bila fujo, ili uonekane kuwa wa huru na haki. Lakini ukweli ni kwamba wamepanga mikakati ya kuwanyika haki wazanzbari wengi fursa ya kupiga kura kwa kuwanyika vitambulisho vya mzanzibari, alisema Maalim Seif.
Aliwataka wananchi, bila kujali tofauti zao za kisiasa, kutokubali kunyimwa vitambulisho vya mzanzibari na kuhakikisha wanapiga kura katika uchaguzi mkuu ujao.
Alisema mipango ya CCM kuhadaa dunia na wananchi ulionekana katika uchaguzi mdogo wa jimbo la magogoni ambako wananchi zaidi ya 1600 walikataliwa kuandiskishwa kwa sababu ya kutokuwa na kitambulisho cha mzanzibari.
Tunataka uchaguzi iliyokuwa huru na haki ili serikali itakayochaguliwa na wananchi iwajali kwa kila mfano kutoa baadhi ya huduma bure. Alisema hivi mpango wa srikali ya Zanzibar kuwalipisha maji wazanzibari ni kuwakandamiza watu masikini, alisema Maalim.
Aidha maalim Seif alisema kuwa wapo baadhi ya wazanzibari wasiotakia mema Zanzibar kutokana na vitendo vyao. Aliwataja watu hao kuwa ni Sheha (viongozi wa mitaa), mkurugenzi wa vitambulisho vya mzanzibari, na mkurugenzi wa tume ya uchaguzi, ambao wanahusika moja kwa moja na mandalizi ya uchaguzi.
Naibu Katibu mkuu Juma Duni Haji, alisema kwamba mkakati wa zinduka, unalenga kuwa zinduwa wananchi kueneldea kudai haki zao kwa njia demokrasia ikiwemo kushirki uchaguzi mkuu ujao.
Aliwataka wananchi kutovunjika moyo na kukata tamaa, kwani kufanya hivyo ni sawa na kuachia shamba nguruwe, huku asisitiza wananchi kujiandikisha.
Pia alituhumu kuwa wapo watu 6000 (elfu sita) wakiwemo maafisa wa tume ya uchaguzi ambao mbali na kuchezea takwimu, kazi yao ni kuchafuwa nchi ya Zanzibar kwa njia mbali. Amemtaka kila mzanzibari kujitolea kwa nafasi yake kupigania haki itakayodumu milele.
Hakuna kudai haki kwa muda mfupi, ni lazima mapambano kuendelea, alisema Duni huku akishitumu ZEC na serikali kuajiri kampuni kutoka Israel kusaidia kuchafuwa uchaguzi mkuu ujao.
Bimani, Duni and Seif waliungana kusema kuwa hakuna kurudi nyuma katika mikakati yao, na kusisitiza, mara hi (2010) hatukubali kunyanganywa ushindi. Tunataka uchaguzi wa haki ili tuheshimu matokeo.
Wakati uandikishaji wa wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao unaanza julai 6 mwaka huu kisiwani Pemba, wafuasi wa CUF waliwemo wajumbe wa baraza la wawakilshi wamekuwa wakilalamika kuwa wafuati wao wanalengwa kunyimwa vitambulisho vya mzanzibari ambavyo vinatakiwa ili kuandiksihwa kupiga kura.
SOURCE: ZANZIBAR YETU BLOG.