Elections 2010 Wakati CUF Ikizindua Mkakati wa Ushindi 2010; CCM Tumbo Joto Z'bar

Junius

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
3,181
139
CHAMA cha wananchi (CUF) kimezindua mkakati mpya unaolenga kushinda uchaguzi mkuu ujao, huku ikitoa tuhuma dhidi ya serikali na Chama cha mapinduzi (CCM) kuhusu undanganyifu.

Katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliyofanyika katika viwanja vya Kibanda-maiti mjini hapa mwishoini mwa wiki iliyopita, viongozi wa chama hicho walizindua “mkakati wa kuelekea Ikulu, na mkakati wa zinduka.”

Katibu mkuu wa CUF maalim Seif Sharif Hamad, Naibu wake Juma Duni Haji, na Mkurugenzi wa uenezi Salum Bimani, kwa nyakati tofauti, waliwataka wafuasi wao kuunga mkono mikakati hiyo kwa kujinadkisha.
“CCM chini ya Rais Kikwete, wamepanga mkakati wa kufanya uchaguzi bila fujo, ili uonekane kuwa wa huru na haki. Lakini ukweli ni kwamba wamepanga mikakati ya kuwanyika haki wazanzbari wengi fursa ya kupiga kura kwa kuwanyika vitambulisho vya mzanzibari,” alisema Maalim Seif.

Aliwataka wananchi, bila kujali tofauti zao za kisiasa, kutokubali kunyimwa vitambulisho vya mzanzibari na kuhakikisha wanapiga kura katika uchaguzi mkuu ujao.

Alisema mipango ya CCM kuhadaa dunia na wananchi ulionekana katika uchaguzi mdogo wa jimbo la magogoni ambako wananchi zaidi ya 1600 walikataliwa kuandiskishwa kwa sababu ya kutokuwa na kitambulisho cha mzanzibari.
“Tunataka uchaguzi iliyokuwa huru na haki ili serikali itakayochaguliwa na wananchi iwajali kwa kila mfano kutoa baadhi ya huduma bure. Alisema hivi mpango wa srikali ya Zanzibar kuwalipisha maji wazanzibari ni kuwakandamiza watu masikini,” alisema Maalim.

Aidha maalim Seif alisema kuwa wapo baadhi ya wazanzibari wasiotakia mema Zanzibar kutokana na vitendo vyao. Aliwataja watu hao kuwa ni Sheha (viongozi wa mitaa), mkurugenzi wa vitambulisho vya mzanzibari, na mkurugenzi wa tume ya uchaguzi, ambao wanahusika moja kwa moja na mandalizi ya uchaguzi.

Naibu Katibu mkuu Juma Duni Haji, alisema kwamba mkakati wa zinduka, unalenga kuwa zinduwa wananchi kueneldea kudai haki zao kwa njia demokrasia ikiwemo kushirki uchaguzi mkuu ujao.
Aliwataka wananchi kutovunjika moyo na kukata tamaa, kwani kufanya hivyo ni sawa na “kuachia shamba nguruwe,” huku asisitiza wananchi kujiandikisha.

Pia alituhumu kuwa wapo watu 6000 (elfu sita) wakiwemo maafisa wa tume ya uchaguzi ambao mbali na kuchezea takwimu, kazi yao ni kuchafuwa nchi ya Zanzibar kwa njia mbali. Amemtaka kila mzanzibari kujitolea kwa nafasi yake kupigania haki itakayodumu milele.
“Hakuna kudai haki kwa muda mfupi, ni lazima mapambano kuendelea,” alisema Duni huku akishitumu ZEC na serikali kuajiri kampuni kutoka Israel kusaidia kuchafuwa uchaguzi mkuu ujao.

Bimani, Duni and Seif waliungana kusema kuwa hakuna kurudi nyuma katika mikakati yao, na kusisitiza, “mara hi (2010) hatukubali kunyanganywa ushindi. Tunataka uchaguzi wa haki ili tuheshimu matokeo.”

Wakati uandikishaji wa wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao unaanza julai 6 mwaka huu kisiwani Pemba, wafuasi wa CUF waliwemo wajumbe wa baraza la wawakilshi wamekuwa wakilalamika kuwa wafuati wao wanalengwa kunyimwa vitambulisho vya mzanzibari ambavyo vinatakiwa ili kuandiksihwa kupiga kura.

SOURCE: ZANZIBAR YETU BLOG.
 
Kichwa cha habari hakiendani na habari yenyewe. Haijasema ni kwa vipi CCM wamekuwa matumbo joto! Halafu hawa CUF inakuwaje wanalalamika kuhusu uchaguzi wa Magogoni wakati walikubali matokeo ya uchaguzi huo? Au wanaanza kujihami ili wapate public sympathy? CUF wamefulia, hawana jipya!
 
wamefanyia visiwani tu au vipi maana na huku Bara vipi jamani
 
Buchanan
Kichwa cha habari hakiendani na habari yenyewe. Haijasema ni kwa vipi CCM wamekuwa matumbo joto! Halafu hawa CUF inakuwaje wanalalamika kuhusu uchaguzi wa Magogoni wakati walikubali matokeo ya uchaguzi huo? Au wanaanza kujihami ili wapate public sympathy? CUF wamefulia, hawana jipya!

Kweli hawana jipa tangu profesa wao aanze kutetea hoja za mafisadi! sasa hivi mkakati wao mkubwa ni hoja ya kusema kwamba Chadema ni CCM-B kwamba chama hicho kinakwezwa na CCM kwa ajili ya kuidhoofisha CUF. Kwa maneno mengine Chadema na CCm ni dam-dam! Ukisika kuchanganyikiwa ndiyo huko!
 
CUF wamepoteza mwelekeo kabisa na itakuwa shinda sana huku Bara kupata public support kubwa mwakani
 
[tumain][]CUF leteni mikakati ya ushindi walau wa majimbo "mawili" bara
Maalimu seif 2010 ndio uwe mwisho wako ikiwa hawatakuchagua naomba upumzike utakuwa una-bore tutakupa shukruni kwa kujaribu kuibua mawazo ya kimapinduzi (kuanzisha) si lazima ule matunda yake..please uwe ni mwisho wako kugombea

Maalim hawezi kuifanya ikawa mwisho kwani sasa hivi kugombea ni mradi mkubwa kwa wakubwa wa CUF.
 
Buchanan

Kweli hawana jipa tangu profesa wao aanze kutetea hoja za mafisadi! sasa hivi mkakati wao mkubwa ni hoja ya kusema kwamba Chadema ni CCM-B kwamba chama hicho kinakwezwa na CCM kwa ajili ya kuidhoofisha CUF. Kwa maneno mengine Chadema na CCm ni dam-dam! Ukisika kuchanganyikiwa ndiyo huko!

Kwa CUF inaonekana kuwa mbaya wao kwa bara ni CHADEMA. Uchaguzi wa Jimbo la Mbeya Vijijini walitumia muda wao mwingi kukilaumu CHADEMA pamoja na kwamba walijitoa kwenye uchaguzi huo wakaiacha CCM ikapeta kiulaini. Kwa ujumla hawana sera zaidi za 'Zanzibar ni nchia au sio nchi!' Haya majina ya Lipumba, Shariff watu wameyachoka, walete sera na nyuso mpya!
 
The reality is CUF ina nguvu visiwani tu na hawana makali yoyote Bara. Chadema kina nguvu zaidi ya CUF Bara kwa sasa na isingekuwa Zanzibar sidhani kama tungekua tunaongelea CUF kwa wakati huu.
 
Wana sera lakani wana matatizo yao na pia huku Bara itakuwa vigumu sana kwao kwasababu huwa wanapoteza muda mwingi sana huku Visiwani na sio kujenga bara
 
CUF is a spent force as far as politics is concerned.They are past their prime.
Dalili za Prof kuingizwa mjini ni baada ya yeye kuwatetea hadharani mafisadi waliomo CCM.Mafisadi hao hata JK hathubutu kukutana nao hadharani.
 
The reality is CUF ina nguvu visiwani tu na hawana makali yoyote Bara. Chadema kina nguvu zaidi ya CUF Bara kwa sasa na isingekuwa Zanzibar sidhani kama tungekua tunaongelea CUF kwa wakati huu.

Laiti wangekubali kushirikiana hawa wakiwa na nguvu visiwani, hawa huku bara, mambo yangekuwa mazuri, Lakini wapi? mafisadi wanajua kwamba ushirikiano huo ukidumu, mwisho wao utakaribia, hivyo kwa garama yoyote ile watahakikisha wanapanda chuki, na mamluki kuhakikisha vyama hivyo vinalumbana vyenyewe badala ya kushirikiana!
 
CUF tangu waambiwe ni chama cha kidini na fujo wameshindwa kabisa kufurukuta. Wanatakiwa watumie nguvu kubwa sana bara ili kuondoa doa hilo. Kuhusu visiwani nafikiri sio visiwa vyote kwamba CUF ni maarufu. Ni Pemba tu ndio CUF wana umaarufu. Nafikiri umaarufu huo unatokana na Seif kuaminiwa mno na wapemba. Kuhusu kushirikiana CUF ndio siku hizi wanataka ushirikiano kwa sababu mambo ni magumu kwao. Siku zote wamekuwa wakijiita chama kikuu cha upinzani na walifikiri wataendelea kuwa hivyo. Muda si muda CUF watakuwa nyuma ya CHADEMA esp kwenye uchaguzi wa mwakani.
 
Junius . huna mpya ndugu yangu. CUF hawawezi kuchukua pale. Siasa zenu - fanyeni- lakini kuna yale ya ustawi wa jamii- Mimi watoto wangu ni wa Mgogoni upande wa mama.
 
Usiponde CUF- Swahib . Ni Chama cha Wa-zanzibari.
 
You nailed it to the point mkuu. CUF siyo chama cha kidini sema kwa sababu viongozi wake wengi ni Waislamu na kwa kuwa nguvu yao ni Zanzibar tu ambao ni 90% Muslim ndiyo maana inaonekana hivyo. Hata isiwe ukweli chama ukishaanza kuwa labelled kama inabidi ifanyike kazi kufuta label hiyo. Na kuhusu CUF kuwa na nguvu Pemba hiyo umeipatia bila ubishi mkuu. CUF ikiendelea kuonekana ni chama cha visiwani tu hawata kuja kushinda uraisi wa Muungano hata siku moja.
 
Junius . huna mpya ndugu yangu. CUF hawawezi kuchukua pale. Siasa zenu - fanyeni- lakini kuna yale ya ustawi wa jamii- Mimi watoto wangu ni wa Mgogoni upande wa mama.
Pakacha hiyo "chorus" tu imeshatawanya panya wote katika kichaka cha kisiwandui, nani mchawi hajuulikani, CUF wanakwenda ki-intelijensia. Subiri utaskia mambo na vijambo karibuni tu.
 
CUF tangu waambiwe ni chama cha kidini na fujo wameshindwa kabisa kufurukuta. Wanatakiwa watumie nguvu kubwa sana bara ili kuondoa doa hilo. Kuhusu visiwani nafikiri sio visiwa vyote kwamba CUF ni maarufu. Ni Pemba tu ndio CUF wana umaarufu. Nafikiri umaarufu huo unatokana na Seif kuaminiwa mno na wapemba.
Fikiria vizuri, CUF(chama cha wananchi si cha kidini) kina umaarufu visiwa vyote vya Unguja na Pemba, kina majimbo ya Uwakilishi kutoka visiwa vyote, kitu ambacho CCM hawathubutu kufanya ni kushinda kiti hata kimoja kisiwani Pemba wakati CUF wana jeuri ya kushinda katika visiwa vyote tokea vyama vingi vianze. Na hata bara CUF imeshawahikuwa na kiti cha uwakilishi bungeni kuonyesha kuwa ni chama cha wananchi wa Tanzania kinachokubalika na wananchi wote bara na visiwani vyama vyengine vyoote vya upinzani havina jeuri hiyo, na huo udini na ukabila ni Propaganda za CCM No.1 na CCM No.2(chadema)
 
CUF wakitaka kushinda wanatakiwa kuikomalia CCM ili muafaka ufikie makubaliano kabla mwaka huu haujaisha. Kama mazingira ni yale yale ya mwaka 2000 na 2005, ni ngumu sana kushinda uchaguzi ama uchaguzi kuwa huru na wa haki.

Tatizo ni kwamba akina Lipumba wameishaanza kula kwenye sahani moja na mafisadi, hapo ndipo wamejimaliza wenyewe na muafaka ndo umezikwa, labda wanachama wachachamae tena kuwataka akina Lipumba na wenzake wang'oke kwa kuwa wameshindwa kazi.
 
Back
Top Bottom