'Wakaresaseya' wahujumu wa kulipwa kumaliza mahusiano usioyoyataka

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,191
4,104
'Wakaresaseya' wahujumu wa kulipwa kumaliza mahusiano usioyoyataka

Utafiti uliofanywa unaonesha kuna karibu matangazo 270 mtandaoni ya makundi yanayotoa huduma hizo, mengi yanahusishwa na makampuni ya ujasusi ya binafsi

Nchini Japan unaweza kulipa kundi binafsi linalojulikana kama 'wakaresaseya' kumtongoza mpenzi wako.

Mwaka 2010, Takeshi Kuwabara alifungwa jela kwa makosa ya kumuua mpenzi wake, Rie Isohata. Lakini kile kilichozua gumzo sio mkasa wenyewe, ni ukweli kwamba
Afisa wa kundi la wakaresaseya kwa jina Kuwabara, ambaye alikuwa ameoa na kujaaliwa watoto, alipanga kukutana na Isohata katika duka la manunuzi.

Alidai kwamba yeye ni mfanyakazi katika kampuni ya Teknolojia na Habari, ambaye pengine muonekano wake ulikuwa na ushawishi mkubwa kwa aliyekuwa anakutana nae. Wawili hao walianza mahusiano, ambayo baadae yalinoga na wakaanza kuishi kama mume na mke.

Wakati huohuo, mfanyakazi mwenza wa Kuwabara akawapiga picha wakiwa kwenye hoteli moja katika mandhari yaliyoashiria mapenzi na mume wa Isohati akatumia picha hizo kama ushahidi wa kutaka kuachana. Ili talaka ikubalike nchini Japan, ushahidi wa aina hiyo ni muhimu.

Isohata alipojua kwamba mume wake alitumia njia za udanganyifu kumuhadaa, alijaribu kuvunja uhusiano wake na Kuwabara afisa yule wa kijasusi aliyekodiwa na mume wake. Lakini kwasababu hakutaka amuache akaamua kumnyonga kwa kutumia kamba. Mwaka uliofuata, akafungwa jela miaka 15 gerezani.

Baada ya kutokea mauaji ya Isohati, kundi la wakaresaseya lilipata pigo, pamoja na visa vya ufisadi, mkasa huo ulifanya kundi hilo kufikiria kuanza kubadilika ikiwemo agizo kuwa yeyote anayefanya kazi hiyo lazima apate kibali cha kuthibitisha kuwa yeye ni jasusi binafsi.

Yusuke Mochizuki, mkuu wa kundi la kijasusi anasema pigo kwanza kukumbana nalo ilikuwa kuondoa tangazo la huduma wanazotoa mtandaoni na kusababisha wasiwasi zaidi kwa umma, waliotaka kundi hilo kuendelea na kazi yake.

Lakini miaka kumi baada ya mauaji ya Rie Isohati, matangazo ya mitandaoni yamerejea tena na inaonekana biashara imeanza kunoga upya, licha ya gharama ya juu ya huduma na mgogoro uliopo kwa uendeshaji wa kazi hiyo.

Imebainika kwamba kuna watu wengi wanaotafuta huduma hiyo wakiwafuatilia wapenzi wao.


Uhitaji wa huduma ya wakaresaseya
Utafiti uliofanywa unaonesha kuna karibu matangazo 270 mtandaoni ya makundi yanayotoa huduma hizo, mengi yanahusishwa na makampuni ya ujasusi ya binafsi sawa na wachuguzi binafsi wa nchi nyingine duniani.

Pia imebainika kwamba kuna watu wengi wanaotafuta huduma ambayo ni kufuatiliwa kwa wapenzi wao.

Mwandishi wa vitabu Scott Stephanie ambaye makao yake ni London, kitabu chake kipya cha 'What's Left of Me Is Yours'' kimezungumzia kisa cha Isohata.

Scott anasema kutafuta huduma kutoka kwa kundi la wakaresaseya kunasaidia kutogombana na mtu. ''Ni namna moja ya kutatua mzozo wa mahusiano kwa njia rahisi. Na mke wake atakuwa na uwezekano mkubwa wa kukubali kutalakiana ikiwa anapenda mtu mwingine na anataka kusonga mbele na maisha yake.

Na huduma hii inakuwa muhimu sana pale mmoja kati ya wawili wanaopendana anapokataa kumtalaki mwingine na kufanya mchakato kuwa mgumu zaidi''.

Lakini wateja wengi sio wale waliooana wanaotaka usaidizi wa kutengana badala yake ni wake na waume wanaotaka kunusuru ndoa zao na kutafuta kila mbinu kumaliza mahusiano ya kando ya mpendwa wake.

Na hapa anaelezea kuihalisia jinsi kazi hiyo inavyotekelezwa.

Tuchukulie kwa mfano, Aya anaamini kwamba mume wake ana mahusiano nje ya ndoa. Kwa hiyo anatafuta huduma kutoka kwa afisa wa wakaresaseya, anayeitwa Chikahide.
Chikahide anaanza kufanya utafiti: Na kuchunguza chochote ambacho ameachiwa na Aya cha kumsaidia kufanikisha lengo la kumfuatilia mpenzi wake Bungo.

Atamfuatilia Bungo hadi kwenye mitandao ya kijamii, kwenye wasifu wake na ujumbe wa simu hadi atakapojua anapenda rafiki wa aina gani na mtindo wake wa maisha.
Anapiga picha na kuthibitisha kwamba kweli kuna udanganyifu. Bungo hupenda sana kufanya mazoezi ya viungo kwa hiyo Chikahide atatuma mwanaume mwingine kwa jina Daisuke, ambaye ana lahaja ya sehemu nyingine ili wakawe marafiki.

Daisuke ataanza kufika kwenye eneo la mazoezi ambako Bungo huwa ni lazima afike kila siku, na kuanza mazungumzo naye kama kawaida hadi awe rafiki yake. Lakini tayari kuna mengi anayoyajua kumhusu Bungo kwasababu alipewa taarifa na Chikahide aliyefanya utafiti.

Soko la wakaresaseya linatazamwa kama mkombozi kwa wengi wale walioajiriwa bila kuwa na leseni


Kwa hiyo ni rahisi hata kwa Daisuke kuanzisha mazungumzo ambayo Bungo huyapendelea na kuonekana kana kwamba kuna mengi yanayofanya wanaume hao wawili kuendana. Na hatimae ataanza kujua kuhusu mchumba wake wa pembeni, kwa jina Emi.

Dausuke sasa ataanza kuleta rafiki wake wa kike Fumika ambaye pia ni jasusi wa kundi hilo. Na kama Daisuke na rafiki yake anayemfuatilia kwenye mazoezi Bungo, Fumika ataanza kutafuta urafiki na Emi hadi atakapojua mengi kumhusu, ikiwemo uhusiano ambao angependelea kuwa nao.

Fumika hatimae ataenda kukutana kwa ajili ya chakula cha jioni lengo likiwa ni Emi, Watakaohudhuria watakuwa ni majasusi wengine wasiojulikana mmoja wao ni Goro.
Goro naye sasa anajua kila kitu kuhusu Emi na anajitokeza kama anayetaka kumchumbia. Goro anamtongoza Emi ingawa mpangaji mkuu yuko makini sana kuhakikisha hakuna jasusi anakuwa na mahusiano ya kweli ya mapenzi na mlengwa kwasababu huko kutakuwa ni kuvunja sheria.

Sasa kwasababu atakuwa na uhusiano na mwanaume mwengine, Emi ataachana na Bungo. Hayo yatakuwa ni mafanikio, ingawa mteja anaweza kurejea tena ikiwa mahusiano hayo yataanza tena.

Goro ataanza kujitoa taratibu kwenye mahusiano bila kuonesha kwamba alikuwa jasusi.

Ili lengo liweze kufikiwa, majasusi wanne wanahitajika na karibu miezi minne hadi uhusiano utakapokuwa umeisha kabisa. "Ni lazima uwe na uelewa wa sheria za Kijapani," anasema mkuu wa kundi hilo. Ikiwemo zile za uhusiano na ndoa, kutalikiana na yale ambayo hustahili kuyafanya kama vile kuvunja uhusiano na kuanza mahusiao mengine moja kwa moja au kuanza kutoa vitisho.

Mikono ya wapenzi

Soko la Japani kwa huduma za mahusiao

Kulingana na mwandishi wa vitabu Scott, ni vigumu sana kujua ni kina nani hasa walioathirika na kundi hilo kwasababu "watu hawapendi kuhusishwa nalo, na waathirika pia hawajitokezi".

Kama mtayarishaji wa vipindi vya kwenye redio na televisheni Mai Nishiyama anavyosema, "Nchini Japan kuna soko la kila kitu." Hayo ni pamoja na familia ya kukodi, na huduma nyingine zinazotolewa na kundi la wakaresaseya kama vile usaidizi wa mwenzako wa kukuomba msahamaha na kurudiana kwa mapenzi moto moto, kutenganisha mtoto wake na mchumba wake ambaye unamuona sio sahihi kwa mwanao.

Pia kundi hilo la majasusi linaweza kutumiwa kusaidia kukusanya ushahidi utakaowezesha mchumba aliyekosewa kupata pesa wakati ambapo mahusiano yamekatika kabisa.
Kuendelea kuwepo kwa kundi la wakaresaseya kunamaanisha kwamba inawezekana watu walio katika mahusiano wakaingiwa na uwoga katika suala zima la kudanganya kwenye mapenzi.

"Ni kazi zuri sana," Mkuu wa kundi hilo anasema. Nimepata uelewa mzuri wa vile watu wanavyodanganya, kutilia chumvi. Kuzungumza na kufasiri mambo. "Inafurahisha sana kuona uhalisia wa mwanadamu."
 
Back
Top Bottom