Wakandarasi wetu sio wetu ni wa China - Asimilia 99.999% ya wakandarasi wetu sio wetu ni wachina

winnerian

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
335
530
Tutaambia nini watu siku tunaingia mgogoro na china! Ni nani atakaye jenga barabara zetu kama hatutakua na wakandarasi wakubwa na wa kuaminika kwa kiwango cha kimataifa. Muundo wa uwezeshaji na dhana nzima ya kuwa na wakandarasi bora bado ni utapeli wa majukwaa ya kisiasa. Unategemea nini kama Taifa halina "jeshi" lake kwa upande wa sekta nyeti kama hiii ya ukandarasi na nyingine nyingi zinazohitaji wataalamu.

Mfano wa sekta ambazo lazima serikali iunde mpango unaoeleweka na kutekelezwa kwa umakini bila rushwa na kiuadilifu sana. Yaani usimamizi uliotukuka; wa kuwaweza sekta binafsi kumudu mambo kadhaa katika taifa letu liwe Taifa la kujitegemea

1. Wataalaamu wa madawa na magonjwa ya binadamu (Sekta binafsi) - Ikibidi serikali iwasomeshe watu wake waje nchini wapewe uwezo wa kutengeneza madawa na vifaa vingine vinavyohitajika mahospatalini.

2. Wanasayansi na wahandisi wa kada mbalimbali - Viwanda bila watalaamu wenye uwezo wa 100% bila siasa ni sawa na uwekezaji wa kinyojaji tu. Maana tunaweza kuwa na viwanda lakini vikamilikiwa na watu kutoka nje

3. Wafanyabiashara katika sekta ya utalaamu kama vile wahandisi washauri, medical consultants, wabia wa sekta mbali mbali zinazohitaji utalaama wanatakiwa kuwezeshwa na serikali hata katika kupewa miradi na tender mbali mbali za serikali ili kujinga uwez wa ndani na sio kuchukua wageni kutoka nje ya Tanzania kisha tunasema kwa mdomo kwamba tunasonga mbele.
 
Bila kuwawezesha wananchi na kuwajengea uwezo waweze kumiliki mitaji kuendana na dunia ya sasa ya uwekezaji na teknolojia, wananchi/watu wetu wataendelea kuwa wasindikizaji. Ni wakati wa kuacha kuangalia maslahi ya chama na kupambania uwepo wa chama baadala yake tujikite kuwainua Watanzania waweze kumiliki mitaji bila ya kuangalia usoni kwa maana ya nani ni nai.. Tusipokuwa makini watu wetu watakuja kuwa watumwa wa WAKENYA, WANYARWANDA, WAGANDA, WAZAMBIA NA WACONGO kwa kushindwa kumiliki mitaji zaidi ya kutegemea mitaji ya wengine ndio wao waishi.
 
Back
Top Bottom