Wakandarasi fake kuhimili mikikimikiki ya wizara ya Magufuli/Mwakyembe? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakandarasi fake kuhimili mikikimikiki ya wizara ya Magufuli/Mwakyembe?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jethro, Nov 25, 2010.

 1. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #1
  Nov 25, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Wana JF,

  Ninge penda sana kuona ufanisi wa wizara ya mindombinu (Dr. Maghufuli & Dr. Mwakyembe) waki deal sana na hawa makandarasi fake huku mikoani kwetu wanavyo tutengenezea barabara mbovu na za kisaanii sana. eg Double Roads za Dodoma mjini anacha na ile iendayo singida, Arusha- Njiro kutokea Impalla Hotel kwenda njiro Temdo, Musoma/Shinyanga mjini Rami za kuunga unga tuu, Babati hadi Singida pia mifano michahche kama wana JF mna ya kuongeza ongezeni

  Maghufuli / Mwakyembe nategemea sana kuona ufanisi wao wa kazi kutokana na uchapaji kazi wao tuuonavyo na kuhakikisha na kusafisha wakandarasi fake.

  Kubwa zaidi tunge penda kujua tamko lao ambalo litawapa imani na uamini kwa wananchi katika wizara hiyo.
   
 2. RasJah

  RasJah JF-Expert Member

  #2
  Nov 25, 2010
  Joined: Nov 5, 2009
  Messages: 697
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  yeah itakuwa poa sana mzee mana hela ipo na mambo yaanze sasa maana mwanzo ndo huu kaka hongera jakaya kikwete na baraza hili naona linatumaini jipya kwa mimi na watanzania ambao wameguswa na uteuzi mimi moja wapo nakubali sana sasa nakuombea kazi njema na serikali njema , peace
   
 3. a

  adobe JF-Expert Member

  #3
  Nov 25, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 1,666
  Likes Received: 290
  Trophy Points: 180
  ka pia kuwa Rombo kwa Mramba ambaye baada ya kukosa Uwaziri aliisusa ile barabara.Ni kama km 15 tu zimesalia lakini ubabaishaji mtupu.DR magufuli, Dr.Mwakyembe angalieni hayamaeneo bila kujali chama gani kinaongoza majimbo
   
 4. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #4
  Nov 25, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Wawasimamie ipasvyo wale wachina waliopewa barabara za kule sumbawanga bse sina imani nao kabisa bila kusahau wale waliopewa ile ya songea kwenda mbinga.
  Alafu kipande kama cha 2km kutoka nyororo kama unaenda makambako just imagine ata mwaka hakijamaliza ni vumbi kwenye highway jamani huu ni uhuni,nadhani Mwakyembe atakiona akiwa naenda jimboni kwake.
  Songwe internationla airport kila siku tunapigwa sound hii nayo haijatulia kuhusu lini utaisha huu uwanja
   
 5. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #5
  Nov 25, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,981
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Ndg yangu Jethro naona hapo patamu. Combination ya hawa jamaa ni moto saana. Makandarasi wasanii,wababaishaji, mafisadi na wengineo wa aina hii watafute pa kwenda. Maana hapo ni full muziki. Hawa waheshimiwa wasiishie barabara za TanRoad tu bali waingie kwenye Halimashauri zetu huko kumeoza na kandarasi feki ni nyingi.Tungoje tamko lao na kazi ianze. Tunawatakia kazi njema isiyo na ufisadi!!! Hongela Dr Magufuli hongela Ndg yangu Dr Mwakyembe.
   
 6. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #6
  Nov 25, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Duuu wataka kuniambia ile barabara na upanuzi wote ule na gharama zote zile wameisusa tena maana ni nzuri sana nilipita may kule khaaaa

   
 7. Cracker Sr

  Cracker Sr New Member

  #7
  Nov 25, 2010
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naamini wadau mko sawa sawia, kama jamaa wakifanya kazi kama 'WALIVYO'!! Mambo yatasonga sasa.
  Hata ile migogoro ya mikataba, mara TANROADS wana kesi Denmark, mara wana kesi Uswisi!! Wakati mambo yetu hayasongi hapa!! Hatutayaona tena. Natamani jamaa waonyeshe njia ya kiutendaji kweli kweli! BIG UP Maguf/MwaK!
   
 8. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #8
  Nov 25, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Hata wakija makandarasi toka S.Africa sikatai hata wakituchukulia kazi maana wa makandarasi wetu hawataki kukuza viwango na kuboresha material yao ya rami. maana S.Africa wana Rami nzuri sn hata usiku huwa ina melemeta sana za hawa wenzetu makandarasi wa kibongo wanao pewa kazi kwa kujuana duuuh zina ongeza Darkness usipaime na barabara unazikuta zina manundu chungu mzima barabar haimalizi miaka miwili ikipigwa na mvua khaaaa rami inaota matobo ni kuwa kulikuwa na nini hata wakaguzi hawaelewi kupima barabara au??

  Jamani tunataka tukihama barabara tuzisahau miaka zaidi ya 10 ni zitafutiwe tu njia za uboreshaji tuuu ili zidumu na kudumu sio kila miaka mitano unatoa rami unaweka nyingine tutakuwa twatwanga maji kwa kinu jamani. viongozi nao watuhurumie kwa kutupiga fix kila mara khaaa maana kuna fix zingine mpaka zime expire wanakuwa hawna za kutudanganyia tena

   
 9. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #9
  Nov 25, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Hapo umenena mkuu maana hawa wajamaa shule imekwenda yaani wasipo tuangusha nchi yao 2015 bila ubishi nawambieni sasa wao wavurunde na wajifanye wana sikia si ha sa za CCM watapotea
   
 10. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #10
  Nov 25, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Point of correction: Ni wizara ya ujenzi.

  Ni kweli mkuu hawa wapigananji natumai hawatatuangusha. Waendelee kulida heshima yao mbele ya umati wa Watanzania wanaowaamini kwa uchapakazi wao kwa kuhakikisha kuwa hakuna ubabaisjahi katika ujenzi wa barabara zetu n.k. Inasemekana kuwa ujenzi wa kiwango duni wa hizi barabara unachangiwa na viongozi wetu kudai 10 % na zaidi kutoka kwa wakandarasi ili wawape tenda. Sasa jamaa wanapeleka tenda ya bei nafuu ili washinde na hapohapo wanatakiwa watoe 10 % kwa vigogo hivyo jamaa hupunguza ubora kwa kufidia hizo pesa walizotoa kama 10 %. Hope Magufuli na Mwakyembe watawamulika hawa viongozi ndani ya wizara yao.
   
Loading...