Wakaguzi wa CAG watinga UDOM....................... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakaguzi wa CAG watinga UDOM.......................

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Rutashubanyuma, Jan 18, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 18, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,564
  Trophy Points: 280
  Mofisa wa CAG kutinga Udom leo
  Monday, 17 January 2011 19:30

  Mussa Juma, Arusha
  MAOFISA kutoka ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) nchini, leo wanaanza kazi ya kuchunguza malalamiko ya malipo ya Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM) na matumizi ya fedha za utawala.

  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovick Utouh akizungumza na waandishi wa habari jana mara baada ya kufunguliwa mafunzo ya wakaguzi wa hesabu za serikali mjini hapa, alisema tayari maofisa wa ofisi yake walianza kazi jana.

  Hatua hiyo, imekuja siku moja tu tangu, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipotembelea chuo hicho, ambacho kimekumbwa na migogoro na kupokea malalamiko ya wahadhiri wa chuo hicho juu ya malipo ya mishahara yao na pia malalamiko ya matumizi ya fedha yasiyoridhisha katika chuo hicho

  " Baada ya kupata maagizo kutoka kwa Waziri Mkuu, leo(jana) maofisa wangu wameanza kukusanya taarifa Wizara ya elimu , Hazina na Kamisheni ya vyuo vikuu kabla ya kesho(leo) kwenda Dodoma"alisema Otouh.

  Otouh alisema baada ya kukamilisha kazi hiyo, watatoa taarifa serikali ili hatua zichukuliwe ili kuhakikisha Chuo Kikuu cha Dodoma kinakuwa shwari.

  "lengo la serikali ni kuona amani na utulivu vinakuwepo UDOM kwani chuo hiki ni muhimu sana kwa Taifa letu "alisema Utouh.

  Awali. akifungua mafunzo ya wiki moja ya wakaguzi wa hesabu za serikali, Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Raymond Mushi, aliwataka wataalamu hao kutumia mafunzo watakayopata kuboresha utendaji wao wa kazi.

  "Mafunzo haya ni muhimu sana kwenu katika kuwajengea uwezo wa kukusanya ushahidi wa kujua thamani ya fedha katika matumizi na uandishi wa ripoti za ukaguzi"alisema Mushi.

  Naye Utouh alisema mafunzo hayo ni sehemu ya program ya kuwajengea uwezo wakaguzi wa hesabu za serikali kwa ushirikiano na mkaguzi mkuu wa nchini Canada.

  Alisema kupitia taasisi ya CCAF ya Canada, wakaguzi wa hesabu za serikali, wamekuwa wakipatiwa elimu na pia kupata fursa ya kwenda nchini Canada katika Jimbo la New Brunwick kujifunza kwa vitendo.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 18, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,564
  Trophy Points: 280
  Huyu Ludovick Utouh kazi imemshinda.....inakuwaje ausbiri kuitwa badala ya yeye kuwa ni mifumo ya kugundua maovu?
   
Loading...