MLEMVYA RASHID
Member
- Aug 1, 2013
- 89
- 11
Mwanzo » Habari
[h=2]Wakaguzi elimu watakiwa kubaini walimu wazembe[/h]
Na Kamili Mmbando
20th February 2014
B-pepe
Chapa
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Consolata Mgimba.
Wakaguzi wa elimu wa kanda nchini, wametakiwa kuhakikisha wanakagua na kubaini walimu wazembe shuleni na kero zinazochangia kushuka kwa elimu nchini.
Wito huo ulitolewa mjini Bagamoyo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Consolata Mgimba, alipofungua semina ya wakaguzi wa shule za msingi, sekondari na vyuo vya ufundi.
Wajibu huu wa wakaguzi wa shule unalenga kusaidia na kuwezesha vyuo na shule zetu kufikia viwango vya elimu vinavyowekwa na wizara, alisema.
Aliongeza: "Ni muhimu kwa wakaguzi wa shule kuongeza ujuzi na maarifa ili wawasaidie walimu kitaalam na kitaaluma katika kuboresha viwango vya ufundishaji."
Naye Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Shule nchini, Merystella Wasena, aliwataka wadau wote wa elimu kuhakikisha wanasimamia elimu katika nafasi zao.
Nataka kuwaambia hii tabia ya walimu ya kufanya kazi kwa mazoea, sasa imefika mwisho hasa kipindi hiki ambacho tuna hitaji Matokeo Makubwa Sasa katika sekta ya elimu, alisisitiza. Alisema mambo mengi yamekuwa yakifanywa na baadhi ya walimu na wakati mwingine kuwapa ujauzito wanafunzi.
Aliwaonya walimu wenye tabia hiyo kuwa hatakuwa na huruma kwa yeyote atakayebainika akifanya hivyo.
CHANZO: NIPASHE