Heshima Kwenu Wakuu!
Jana bwana nilikuwa natoka zangu nyumbani naelekea maeneo ya Tazara Kutafuta rizki.Nikiwa kwenye kijigari change ka mkopo,nikiwa kwenye foleni maeneo ya tabata mataa,akatokea askari wa usalama barabarani na kuniomba leseni.Bila hiana nikampa leseni.Yule askari akaniambia nipaki gari pembeni alafu nimfuate kwenye kile kijumba chao.Nilipoenda akanitolea receipt kwenye zile POS zao inaonyesha gari langu linadaiwa 120K.Ambapo makosa ni mawili na fine juu.Kuangalia ikaonekana makosa ayo yalifanywa Kimara Kibo mnamo tarehe 01.12.2017.Number ya gari ni yangu ila leseni number ni ya mtu mwingine na mpaka jina lake liko.
Ukweli ni kwamba mda huo ambao kosa lilifanyika(saa tisa) nlikuwa ofisini.
Ikanibidi niwe mkali nikawaambia mwenye leseni simjui kama vipi wamtafute wao alafu tujue kama ni kweli ni gari langu lilitumika kwenye leseni iyo.
Sasa wakuu naombeni ushauri nini cha kufanya maana siku zinavyoenda deni ambalo si langu linazidi kukuwa.