GE2025 Wajumbe wampitisha Morris Makoi ubunge Jimbo la Moshi Vijijini

GE2025 Wajumbe wampitisha Morris Makoi ubunge Jimbo la Moshi Vijijini

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Wajumbe katika Jimbo la Moshi Vijijini wametiki na nakumpitisha Morris Makoi nakupita katika kura za Maoni Jimbo la Moshi Vijijini wapi Prof. Ndakidemi?

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini, Prof. Patrick Ndakidemi, ameshindwa kutetea nafasi yake ya Ubunge baada ya Moris Makoi kuibuka mshindi katika kura za maoni za CCM kwa kupata kura 2,148 kati ya kura halali 4,649 zilizopigwa. Matokeo hayo yametangazwa usiku wa Agosti 4, 2025 na Msimamizi wa Uchaguzi wa CCM Wilaya ya Moshi Vijijini, Ramadhani Mahanyu, ambaye amesema kuwa kura 60 zimeharibika.

Makoi amewashinda wapinzani wake kwa tofauti kubwa, akifuatiwa na Prof. Ndakidemi aliyepata kura 627, Felista Njau (587), Salim Kikeke (491), Victor Tesha (409), Deogratius Mushi (225) na Wilhard Kitaly (102). Matokeo hayo yalitangazwa katika Ofisi za CCM Wilaya ya Moshi Vijijini.
IMG_20250804_184525_441.jpg
 
Prof ndakidemi aligoma jimbo kugawanywa, wajumbe wamemjibu
Alikuwa anajiamini vipi wakati kulikuwa na viashiria kuwa asingetoboa? Alipaswa kujifunza kwa uchaguzi wa 2020. Kuna siku wakati stori za hapa na pale zinapigwa alijisahau akajikuta ameropoka........ kuwa 2020 bila mbeleko asingetoboa.
 
Back
Top Bottom