Wajumbe: Wagombea wanashindana kwa kutumia pesa

Wajumbe: Wagombea wanashindana kwa kutumia pesa

Mtarban

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2015
Posts
3,952
Reaction score
5,263
Wiki iliyopita nikiwa natoka kwenye shughuli zangu ghafla nilikutana na watu watatu, wawili wakiwa wamevalia mashati ya kijani. Kwa mavazi yao na maongezi Yao, fikra zangu zilinipelekea kuwaza kuwa hawa ni "WAJUMBE'

Maongezi yao yalinivutia yakafanya nizidi kuwasikiliza. Kwa ufupi walikuwa wakidai kuwa walichofanya wagombea au watu waliotia nia ni kushindanisha pesa na siyo uwezo ama Hoja zao. Mmoja anadai kuwa aliyekuwa anamsapoti hajashinda kwa sababu wengine wametumia nguvu pesa.

Mwenzao anawajibu kuwa sasa kama mtu ni maskini ukimchagua huyo mtu atawaza umaskini wake Kwanza ataumalizaje hivo Ni Bora kumpa mtu ambaye tayari ana pesa. Baada ya hapo niliyaacha WAJUMBE' wakaelekea makwao na Mimi nikaelekea kwangu.

Ujumbe kwa vijana ambao najua wengi wenu mna uwezo wa kuongoza ila mnakosa uwezo wa kifedha, A asikuambie mtu pesa ina nguvu sana kwenye siasa na inaweza kubadilisha upepo kwa nmna yoyote ile.
 
Back
Top Bottom