Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 5,527
- 7,121
Watu wengi katika dunia hii wanatamani 'kung’aa' kwa umaarufu, heshima, kusifiwa na kupongezwa na wanadamu. Wengine wanatumia pesa nyingi kutafuta urembo, mavazi ya bei ya juu, magari ya kifahari, elimu ya kiwango cha PhDs au hata nguvu ili waonekane juu kama nyota. Lakini ukweli ni kwamba, mtu akiwa nyota katika dunia hii, mwangaza wake hufifia baada ya muda mfupi. Fahari ya kidunia huisha kama kivuli cha jioni.
Leo Mungu anatufunulia jinsi tunavyoweza kuwa miongoni mwa watu watakaong'aa milele na milele. Maandiko yanasema katika Danieli 12:3 "Na walio na hekima watang'aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutenda haki watang'aa kama nyota milele na milele.”
Hao sio watu wanaotafuta umaarufu wa kidunia, bali ni wale wanaofanya bidii kuwaelekeza wengine kuenenda katika njia ya haki. Kwa maisha yao, tabia zao na maneno yao, wanawaongoza wengine kutenda mapenzi ya Mungu. Thawabu yao ni utukufu wa kudumu—kung’aa kama nyota milele na milele katika Ufalme wa Mungu. Hiyo ni ahadi isiyo na shaka kutoka kwa Mungu aliyetuumba, na Yeye hadanganyi.
Jihoji sasa: Unaiongozaje familia yako? Unawaelekeza watoto wako kutenda mema? Kama wewe ni boss kazini kwako, je, wafanyakazi wako unawaongoza kutenda haki? Vipi kijiweni kwako, unawaongoza wenzako kutenda mema au uovu? Jiulize tena: Je, utakuwa miongoni mwa wale watakaong’aa milele na milele katika utukufu wa Mungu, au utakuwa miongoni mwao watakaotupwa katika giza la nje?
"Ndipo mfalme akawaambia watumishi wake, 'Mfungeni miguu na mikono mkamtupe nje gizani; huko atalia na kusaga meno.'” (Mathayo 22:13).