Wajue viumbe wa ajabu waishio angani

Kanungila Karim

Verified Member
Apr 29, 2016
16,576
2,000

MPENZI mwanajamiiforums ungana nami katika simulizi hii mpya ya kweli inayohusu viumbe wa ajabu waishio angani. Kama ni msomaji wa vitabu vitakatifu, Mungu aliumba vitu vinavyoonekana na visivyoonekana. Inahisiwa kuwa visivyoonekana ni vingi kuliko vinavyoonekana.

Viumbe hao wa ajabu waishio angani wanaitwa Aliens. Wana muonekano kama binadamu isipokuwa hawafanani moja kwa moja na binadamu. Viumbe hao waliogundulika karne kadhaa zilizizopita wameshatengenezewa filamu nyingi na wasanii mbalimbali duniani (tutazichambua huko mbele).Aliens wapo wa rangi tofauti kama kijani, weupe, weusi, njano, zambarau na kila aina ya rangi.

Inaaminika kuwa Aliens wanaoishi angani wana akili nyingi kuliko binadamu. Wana mfumo wa kompyuta uitwao Alien Software na wapo juu kiteknojia kuliko binadamu tatizo tuu hawavai nguo!!

Tofauti na binadamu ambaye anafanya kazi kwa hatua moja kwenda nyingine, Aliens wao hufanya mambo kinyume kabisa. Kwa mfano wakitaka kusema ‘naomba maji’ husema ‘maji naomba’ yaani cha nyuma kinakwenda mbele na cha mbele kinarudi nyuma. Kama tunavyowashangaa, nao pia wanatushangaa na kutuona viumbe wa ajabu.

Wachambuzi wa mambo ya anga walishaandika ripoti nyingi kuhusu viumbe hao ambao huja duniani na kurudi angani.

Swali ni je, viumbe hao wanaishi katika sayari gani? Wataalam hao wanalijibu swali hilo kwa kusema haijulikani moja kwa moja wanaishi sayari gani lakini kwa uhakika siyo kwenye mwezi (kumbuka mwezi siyo sayari).
Inawezekana bado hujaelewa simulizi hii. Bermuda Triangle ni eneo la pembetatu la bahari lililopo kati ya nchi tatu katika Bahari ya Atlantiki. Miaka kadhaa huko nyuma viumbe hao waliwahi kutua eneo hilo na kuweka historia (nitaisimulia huko mbele).

Pia waliwahi kuonekana Kisiwa cha Bermuda pwani ya Mashariki mwa Marekani, Kisiwa cha Puerto Rico kilichopo Kaskazini mwa Carrebian na Fort Lauderdale huko Florida, Marekani.

Umewahi kusikia vitu mbalimbali duniani vikisemekana vimepotea katika mazingira ya kutatanisha? Aliens wanahusishwa na upoteaji wa meli baharini hasa za mizigo huku watu wakiamini huwa zinazama lakini uchunguzi ukifanyika meli hizo huwa hazionekani hata ndani ya maji baharini.

Aliens wanatajwa kuhusika na upotevu wa watu duniani ikiaminika kuwa labda watu hao walikufa lakini ukweli ni kwamba huchukuliwa na viumbe hao.
Ndege za kijeshi zimeripotiwa mara nyingi kupotea au kutokuonekana milele katika eneo la Bermuda Triangle ikieleza kuwa Aliens ndiyo wahusika wa upotevu huo.

Ujio wa Aliens katika eneo la Bermuda Triangle ulisababisha kisiwa hicho kupata umaarufu duniani na kupewa jina la Devil’s Sea (Bahari ya Shetani) ambapo binadamu wamekuwa wakiamini au kujenga imani potofu kuwa shetani amekuwa na makazi katika eneo hilo na kuwapoteza wasafiri wa majini. Wengine huhisi ni ushirikina.

Wapo binadamu wanaoamini kuwa Aliens walikuwepo duniani tangu enzi hizo kabla ya binadamu na hawajaondoka.
Si sehemu hizo pekee lakini wamekuwa wakitua maeneo mbalimbali duniani na kuna baadhi ya serikali duniani zinawajua.
Wataalam wa anga wanadai Aliens wako mbali kimaendeleo na wanafanya wanavyotaka.

Je, hawa ni viumbe gani? Ndiyo kwanza simulizi imeanza.
INAENDELEA
 
py thon

JF-Expert Member
Sep 11, 2016
2,469
2,000
Hakuna cha alliens wala cha nini

Hakuna aliyewahi kumuona alliens ni kama vile dhana ya popobawa au nguva ..

Kama alliens wapo mbona hakuna uthibitisho wa picha au video.

Hata dinassour pia ni dhana ..

Alliens,popobawa,dinassours,nguva kiuhalisia hawapo bali wametungwa tu na wanaadamu ..miaka yote tunasikia nguva,alliens,popobawa lkn picha zao hatuzioni
 
Philipo D. Ruzige

Verified Member
Sep 25, 2015
6,426

Ungekua mwanajiolojia, palaentilogist, ungejua mengi kuhusu Dinosaurs, (kasome geological time scale)
Kasome kuhusu mabaki ya hao wanyama yaliyopatikana duniani ikiwepo tanzania pia. Yule mjusi wetu alieko ujerumani

Popobawa limekaa kishirikina na kiroho zaidi, nguva yupo ila sio yule kama mwanamke(nguva ni samaki anayenyonyesha)

Hii kesi ya alliens bado inaniweka njia panda, sometimes naamin sometimes siamin

Ila huwa nawazia hiz Unidentified Flying Objects (UFO) ni vitu gan, mana ufo zimeshaonekana sana ila ndio not identified, so orign yake ni nini, hap ndo napata was was isije kuwa hizi stor za alliens ni kweli.
 
Habibu B. Anga

Verified Member
May 7, 2013
6,656
2,000
Mkuu nilitegemea labda ungeandika argument za kuthibitisha uwepo wa aliens, badala yake umeandika na kusimulia kana kwamba ni kitu halisi kabisa ambacho kimethibitika bila mashaka..

Hao aliens wapo kwenye science fiction stories tu but kiuhalisia hakuna mwenye ushahidi juu ya uwepo wao..

Kisayansi, kuna uwezekano fulani kukawa na uhai katika sayari nyingine zilizopo galaxy nyingine lakini sio kwa namna hii uliyo simulia.!

Anyways, nasubiria muendelezo..
 
HR 666

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
3,936
2,000

MPENZI mwanajamiiforums ungana nami katika simulizi hii mpya ya kweli inayohusu viumbe wa ajabu waishio angani. Kama ni msomaji wa vitabu vitakatifu, Mungu aliumba vitu vinavyoonekana na visivyoonekana. Inahisiwa kuwa visivyoonekana ni vingi kuliko vinavyoonekana.

Viumbe hao wa ajabu waishio angani wanaitwa Aliens. Wana muonekano kama binadamu isipokuwa hawafanani moja kwa moja na binadamu. Viumbe hao waliogundulika karne kadhaa zilizizopita wameshatengenezewa filamu nyingi na wasanii mbalimbali duniani (tutazichambua huko mbele).Aliens wapo wa rangi tofauti kama kijani, weupe, weusi, njano, zambarau na kila aina ya rangi.

Inaaminika kuwa Aliens wanaoishi angani wana akili nyingi kuliko binadamu. Wana mfumo wa kompyuta uitwao Alien Software na wapo juu kiteknojia kuliko binadamu tatizo tuu hawavai nguo!!

Tofauti na binadamu ambaye anafanya kazi kwa hatua moja kwenda nyingine, Aliens wao hufanya mambo kinyume kabisa. Kwa mfano wakitaka kusema ‘naomba maji’ husema ‘maji naomba’ yaani cha nyuma kinakwenda mbele na cha mbele kinarudi nyuma. Kama tunavyowashangaa, nao pia wanatushangaa na kutuona viumbe wa ajabu.

Wachambuzi wa mambo ya anga walishaandika ripoti nyingi kuhusu viumbe hao ambao huja duniani na kurudi angani.

Swali ni je, viumbe hao wanaishi katika sayari gani? Wataalam hao wanalijibu swali hilo kwa kusema haijulikani moja kwa moja wanaishi sayari gani lakini kwa uhakika siyo kwenye mwezi (kumbuka mwezi siyo sayari).
Inawezekana bado hujaelewa simulizi hii. Bermuda Triangle ni eneo la pembetatu la bahari lililopo kati ya nchi tatu katika Bahari ya Atlantiki. Miaka kadhaa huko nyuma viumbe hao waliwahi kutua eneo hilo na kuweka historia (nitaisimulia huko mbele).

Pia waliwahi kuonekana Kisiwa cha Bermuda pwani ya Mashariki mwa Marekani, Kisiwa cha Puerto Rico kilichopo Kaskazini mwa Carrebian na Fort Lauderdale huko Florida, Marekani.

Umewahi kusikia vitu mbalimbali duniani vikisemekana vimepotea katika mazingira ya kutatanisha? Aliens wanahusishwa na upoteaji wa meli baharini hasa za mizigo huku watu wakiamini huwa zinazama lakini uchunguzi ukifanyika meli hizo huwa hazionekani hata ndani ya maji baharini.

Aliens wanatajwa kuhusika na upotevu wa watu duniani ikiaminika kuwa labda watu hao walikufa lakini ukweli ni kwamba huchukuliwa na viumbe hao.
Ndege za kijeshi zimeripotiwa mara nyingi kupotea au kutokuonekana milele katika eneo la Bermuda Triangle ikieleza kuwa Aliens ndiyo wahusika wa upotevu huo.

Ujio wa Aliens katika eneo la Bermuda Triangle ulisababisha kisiwa hicho kupata umaarufu duniani na kupewa jina la Devil’s Sea (Bahari ya Shetani) ambapo binadamu wamekuwa wakiamini au kujenga imani potofu kuwa shetani amekuwa na makazi katika eneo hilo na kuwapoteza wasafiri wa majini. Wengine huhisi ni ushirikina.

Wapo binadamu wanaoamini kuwa Aliens walikuwepo duniani tangu enzi hizo kabla ya binadamu na hawajaondoka.
Si sehemu hizo pekee lakini wamekuwa wakitua maeneo mbalimbali duniani na kuna baadhi ya serikali duniani zinawajua.
Wataalam wa anga wanadai Aliens wako mbali kimaendeleo na wanafanya wanavyotaka.

Je, hawa ni viumbe gani? Ndiyo kwanza simulizi imeanza.
INAENDELEA
Mkuu huo ni mkakati wa devil worshippers ili wateke akili za binadamu
 
Sakasaka Mao

JF-Expert Member
Sep 29, 2016
6,028
2,000
Hakuna cha alliens wala cha nini

Hakuna aliyewahi kumuona alliens ni kama vile dhana ya popobawa au nguva ..

Kama alliens wapo mbona hakuna uthibitisho wa picha au video.

Hata dinassour pia ni dhana ..

Alliens,popobawa,dinassours,nguva kiuhalisia hawapo bali wametungwa tu na wanaadamu ..miaka yote tunasikia nguva,alliens,popobawa lkn picha zao hatuzioni
Hapo kwenye dinossours umechemka. Ni umbumbumbu kiwango cha lami unaokinzana hata na elimu duni ya std lV.
 
Ludanha

JF-Expert Member
Jan 24, 2014
553
1,000
Ungekua mwanajiolojia, palaentilogist, ungejua mengi kuhusu Dinosaurs, (kasome geological time scale)
Kasome kuhusu mabaki ya hao wanyama yaliyopatikana duniani ikiwepo tanzania pia. Yule mjusi wetu alieko ujerumani

Popobawa limekaa kishirikina na kiroho zaidi, nguva yupo ila sio yule kama mwanamke(nguva ni samaki anayenyonyesha)

Hii kesi ya alliens bado inaniweka njia panda, sometimes naamin sometimes siamin

Ila huwa nawazia hiz Unidentified Flying Objects (UFO) ni vitu gan, mana ufo zimeshaonekana sana ila ndio not identified, so orign yake ni nini, hap ndo napata was was isije kuwa hizi stor za alliens ni kweli.
Hakuna cha alliens wala cha nini

Hakuna aliyewahi kumuona alliens ni kama vile dhana ya popobawa au nguva ..

Kama alliens wapo mbona hakuna uthibitisho wa picha au video.

Hata dinassour pia ni dhana ..

Alliens,popobawa,dinassours,nguva kiuhalisia hawapo bali wametungwa tu na wanaadamu ..miaka yote tunasikia nguva,alliens,popobawa lkn picha zao hatuzioni
Msome nguva hapo Ukweli kuhusu Nguva (Samaki mtu)?
 
TIASSA

JF-Expert Member
Jun 17, 2014
2,307
2,000
Hakuna cha alliens wala cha nini

Hakuna aliyewahi kumuona alliens ni kama vile dhana ya popobawa au nguva ..

Kama alliens wapo mbona hakuna uthibitisho wa picha au video.

Hata dinassour pia ni dhana ..

Alliens,popobawa,dinassours,nguva kiuhalisia hawapo bali wametungwa tu na wanaadamu ..miaka yote tunasikia nguva,alliens,popobawa lkn picha zao hatuzioni
Bora hata dinassorr mabaki take yapo museum ila hao wengine sidhani
 
py thon

JF-Expert Member
Sep 11, 2016
2,469
2,000
Hapo kwenye dinossours umechemka. Ni umbumbumbu kiwango cha lami unaokinzana hata na elimu duni ya std lV.
Wanasayansi wanasema Dinosaur walikuwepo miaka million 243 iliyopita , kisha miaka million 66 walipotea

Lakini Leo hii kupitia mifupa wanayosema ni ya dinosaurs wameweza kuwa classify kwa makundi mbali mbali ,wameeleza namna walivyokuwa wanazaliana na facts nyingi bla bla
.
Ishu ya Dinosaurs ni kuwashika watu akili tu na kuwapumbaza ,wao wanadai species hiyo ilitoweka miaka million 60 huko how come wajue mambo kibao kuhusu huyo mnyama

Pia mifupa ikikaa muda mrefu lzm ingepoteza uhalisia wake ,miaka million60+ mifupa si inachakaa kabisa hapo

Haha Yale yale binaadamu wa kwanza nyani ..
 
ivunya

JF-Expert Member
Sep 18, 2015
1,614
2,000
Hakuna cha mwendelezo wowote, hao ni mashetani devils watumika kaleta uongo duniani. Heti wanaongea kinyume sijajua ni lugha gani waliyokuwa wanatumia kuwasliana. Kwenye kiingereza kuna PASSIVE NA ACTIVE. Mtenda anaweza kutangalia akafuata Mtendwa ni sawasawa na kuanza na mtendwa akafuata mtenda.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom