Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,242
- 34,917
Kwa mujibu wa PGO 198(4&5), dereva wa polisi anatakiwa kutekeleza wajibu ufuatao:
(a) Kuendesha kwa usalama na kufuata taratibu zilizowekwa na sheria na kanuni za usalama barabarani;
(b) Kuendesha kwa kujali na kuwa mfano mzuri kwa umma;
(c) Kuzuia watu wasioruhusiwa kuharibu magari ya polisi;
(d) Kutozidisha mzigo kwenye gari na kuubeba mzigo kiusalama
(e) Kuripoti ajali;
(f) Kutoruhusu mtu aisyehusika kuendesha gari la polisi;
(g) Kutoendesha gari analojua kuwa ni bovu;
(h) Kutobeba mtu au mzigo usioruhusiwa;
(i) Kutoliacha gari bila uangalizi;
(j) Kutovuta sigara kazini au karibu na gari;
Pia madereva wa polisi wanaruhusiwa kuendesha magari yasiyo ya polisi au ya serikali ya daraja linaloendana na leseni zao.
Aidha ni marufuku kwa askari asiye na leseni inayotakiwa kuendesha gari la polisi(PGO 197(9). Polisi wenye leseni za muda/lena wanaweza tu kuendesha magari ya polisi wakiwa chini ya maelekezo maalumu.
Aidha, ni marufuku kwa magari ya polisi kuendeshwa kwa speed kubwa (excessive speed) isipokuwa tu pale kunapokuwa na dharula au katika kumfukuza muhalifu au kunapokuwepo na sababu za ulazima wa kufanya hivyo.[PGO 197(10)]
Kwa ufupi ndio kusema kwamba, sio tu raia bali pia, askari hushtakiwa. Hivyo tutii sheria bila shuruti.