Wajiambukiza Ukimwi ili Wapate Msaada wa Pesa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wajiambukiza Ukimwi ili Wapate Msaada wa Pesa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Nov 27, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 27, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Thursday, November 24, 2011 3:37 AM
  Hali ngumu ya maisha nchini Ugiriki imepelekea idadi ya waathirika wa ukimwi nchini Ugiriki iongezeke kwa kasi kutokana na baadhi ya watu kujiambukiza kwa makusudi ukimwi ili wapate pesa zinazotolewa kama msaada kwa waathirika wa ukimwi. Ili waweze

  kupata msaada wa euro 700 zinazotolewa kila mwezi kwa waathirika wa HIV nchini Ugiriki, watumiaji wa madawa ya kulevya wamekuwa wakijiambukiza kwa makusudi virusi vya ugonjwa huo ili waweze kupata msaada huo kila mwezi.

  Ndani ya mwaka mmoja idadi ya waathirika wa HIV nchini Ugiriki imeongezeka kwa asilimia 1260.

  Waziri wa afya wa Ugiriki, Andreas Loverdos alisema "Watumiaji wa madawa ya kulevya ili waweze kupata msaada wa euro 700 kwa mwezi wamekuwa wakiwatafuta watu walioathirika na kujidunga sindano walizozitumia ili na wao waathirike waweze kupata msaada huo".

  Mwaka huu pekee, jumla ya watumiaji wa madawa ya kulevya 190 wamegundulika wameambukizwa HIV na kuanza kupewa msaada huo wa euro 700 kila mwezi.

  Magazeti ya Ugiriki yaliandika taarifa hii ya wizara ya afya kwenye kurasa zake za mbele yakilaumu hali ngumu ya uchumi kuwa ndio iliyochangia kutokea kwa hali hii.

  Chanzo. Wajiambukiza Ukimwi ili Wapate Msaada wa Pesa

  DUNIANI KWELI KUNA MAMBO WAGONJWA WANAOMBA KILA SKU KWA MWENYEEZI MUNGU ILI WAPONE HAYA WAZIMA WANAJIPA MAGONJWA ILI WAPATE MISAADA WA KIFEDHA KWELI DUNIA NI UWANJA WA FUJO KASHESHE KWELI
   
Loading...