Waiting forever

Waiting forever

Say whotevr u deem fit,
im 100 sure God wont grant,
U cnt call back an arrow after u hav shot it,
U messed up with the gift,
Said u havent toiled to get it,
Its gone u hav 2 accept,
Im just sorry for yo unproductv effort,
Wasted wash hands while ts heart wchc is dirty...

Surely you place me on slippery ground;
you've casted me down to ruin.
You're waiting for How suddenly am getting destroyed,
completely sweeping away my loving heart,
As a dream when one awakes, and here I arise,
I will despise them as fantasies.

When my heart was grieved and my spirit embittered,
I was senseless and ignorant;
I was a brute beast before you.
And, Yet I am always with you; (in my heart)
I wanted u to hold me by ur right hand.
guide me with your counsel,
and afterward you will take me into glory.
But all those things in vain.
Poor me.
 
saluni.jpg

Dawa za kulainisha nywele (relaxer) zimekuwa zinapendwa na wanawake wengi wa Afrika kwa kuwa zina uwezo wa kulainisha nywele na kumfanya apendeze na awe wa kuvutia.

Hata hivyo, wataalamu wa afya wanadai kuwa dawa hizo zinasababisha uvimbe kwenye kizazi kutokana na kemikali za dawa hizo ambazo huingia mwilini kupitia majeraha au ngozi wakati wa kupaka.

Daktari wa Manispaa ya Ilala, Laurent Chipata alifanya utafiti na kubaini kuwa dawa za nywele na vipodozi zina kemikali ambazo husababisha uzalishwaji wa vichocheo kwa kiasi kikubwa na kusababisha uvimbe kwenye kizazi uitwao fibroids au leimyoma.

“Kemikali hizi hupenya kwenye ngozi na wakati mwingine hata kwa harufu tu, husababisha kuzalishwa kwa wingi wa vichocheo aina ya estrogen ambavyo huchangia kuota kwa uvimbe wa fibroids,” anasema.

Dk Chipata anasema kukua kwa uvimbe kwenye kizazi hutokea katika kipindi ambacho mama yupo kwenye uzazi yaani kabla hajakoma hedhi.

Utafiti wa Dk Chipata ulifanywa nchini na kujumuisha wanawake wa kada tofauti tofauti wanaotumia dawa za nywele na wale wasiotumia na ukubwa wa tatizo hili ulibainika.

“Zipo kemikali tofauti tofauti zinazosababisha uvinbe kwenye kizazi, zipo za kwenye dawa za kilimo kama DDT na za kwenye mafuta ya ngozi kama vile mercury na hydroquionone,” anasema.

Dk Chipata anasema madhara yanayopatikana katika kemikali za vipodozi ni makubwa siyo tu kwenye kizazi bali nyingine husababisha saratani au kufeli kwa figo. Anatoa mfano wa kemikali ya zebaki (mercury).

“Dawa za nywele zina madhara si lazima zipenye kwenye ngozi baada ya mtu kupata jeraha la kuungua bali zinaweza kupenya zenyewe kwenye ngozi kutokana na mfumo wa ngozi,” anasema.

Anashauri kuwa ni vyema watu wakasoma kipodozi kimetengenezwa kwa nini kabla ya kukitumia na kuongeza kuwa ni salama zaidi kubaki na ngozi au nywele halisi badala ya kujibadilisha.

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imekataza vipodozi vyenye kemikali kama biothionol, hexachlorophene, mercury, vinyl chloride, zirconium na bidhaa zenye aerosol, chloroquionone, steroids, methylene na chloroform.

Utafiti mwingine uliofanywa mwaka 2012 na Dk Lauren Wise na wenzake nchini Marekani na kuchapishwa kwenye jarida la afya la nchini Marekani ulibaini kuwa vipodozi vingi vina kemikali zenye vichocheo vya estrogen ambavyo kwa kawaida huchochea kasi ya kuota kwa uvimbe kwenye kizazi cha mwanamke na wakati mwingine kwenye mji wa mimba. Kitaalamu uvimbe au vivimbe hivi hujulikana kama fibroids au myoma.
Dk Wise anasema aliwafanyia uchunguzi wanawake wanaotumia dawa za kulainisha nywele na kuangali umri walioanza kutumia dawa hizo, mara ngapi, waliungua kiasi gani na walikaa na dawa hizo kichwani kwa kipindi gani.

Aliwafuatilia wanawake 23,580 wanaotumia dawa za kulainisha nywele na baada ya kipindi fulani walipimwa. Kati yao, 7146 waligundulika kuwa na uvimbe kwenye kizazi baada ya kupimwa kwa mionzi na wengine kufanyiwa upasuaji.

Kwa nini relaxer ni hatari kwa wanawake?
Dk Wise anasema mchanganyiko ulio kenye dawa za nywele hasa zilizoandikwa “Lye Relaxer” ni sodium hydroxide wakati makopo ya dawa yaliyoandikwa “No Lye Relaxer” yana calcium hydroxide na guanidine carbonate.

Bidhaa za kulainishwa nywele zilizoandikwa ‘no lye relaxer’ zinadaiwa kusababisha majeraha kwa kiasi kidogo ukilinganisha na zile zilizoandikwa “Lye Relaxer”.

Uvimbe kwenye kizazi ni nini?
Ukuta wa nyumba ya uzazi umejengwa kwa misuli ya tishu. Kwa kawaida uvimbe huu huanza kidogo kidogo na hukua hadi kufikia ukubwa wa tikiti maji. Fibroids kubwa huweza kukua na kutanua nyumba ya uzazi na kuwa sawa na ujauzito wa miezi sita au saba.

Mwanamke huweza kuwa na uvimbe mmoja mkubwa au vivimbe vingi ndani ya kizazi.
Daktari Bigwa wa magonjwa ya uzazi wa Kitengo cha Upasuaji cha Chuo Kikuu Sayansi ya Tiba Muhimbili, Henry Mwakyoma anauelezea fibroids ni uvimbe ambao upo katika umbile la misuli myembamba na laini linalokua siku hadi siku.

“Sababu inayopewa kipaumbele zaidi ni wingi wa vichocheo vya estrogen ambavyo vipo katika miili ya wanawake,” anasema.

Dk Mwakyoma anafafanua kuwa, vichocheo hivi ndivyo hufanya kazi katika mwili wa mwanamke na kumsababishia kupata siku zake za hedhi.

“Ndiyo maana wengi wanaopata uvimbe huu, huwa ni wanawake walio katika umri mkubwa au ambao tayari wamevunja ungo, kwani ndiyo ambao huzalisha vichocheo vya estrogeni,” anabainisha mtaalamu huyo.

Dalili za uvimbe wa Kizazi

“Dalili hutegemeana na eneo ulipokaa uvimbe na ukubwa wake. Wengi hugundulika wakati wa kujifungua au endapo mwanamke atapata uvimbe katikati ya kizazi, basi huweza kutokwa damu kwa wingi,” anasema.


Anaongeza: “Hata hivyo, asilimia 35 hadi 50 ya wanawake wanaougua maradhi haya huonyesha dalili wakati wa kujifungua,”

Dalili nyingine ni mwanamke kutokwa damu zake za hedhi kwa wingi na kwa siku nyingi. Damu za hedhi huweza kuwa nyingi au kidogo sana zikiambatana na maumivu makali.

Anasema wakati mwingine mwanamke huweza kuhisi ana ujauzito kwani uvimbe huu huwa mkubwa na huchezacheza kana kwamba ni kiumbe.

“Nina mifano hai, wapo wanawake waliowahi kuhisi wana ujauzito, wakakosa kabisa siku zao za hedhi, wakaona dalili zote za mimba na kumbe walikuwa na uvimbe wa fibroids,” anasema.

Msemaji wa TFDA, Gaudensia Simwanza anasema wamekuwa wakifanya ukaguzi mara kwa mara kuzuia uuzwaji wake.

Isitoshe akasema: “Elimu inatolewa kwa wananchi pia ili kuwafahamisha kuhusu madhara ya vipodozi hivyo kwa sababu wanunuzi wasipokuwepo basi hata biashara haitakuwepo.”

Pamoja na hayo, adhabu hutolewa ya kuwanyang’anya na kuwapeleka mahakamani wenye maduka makubwa wakiziuza.
 
saluni.jpg

Dawa za kulainisha nywele (relaxer) zimekuwa zinapendwa na wanawake wengi wa Afrika kwa kuwa zina uwezo wa kulainisha nywele na kumfanya apendeze na awe wa kuvutia.

Hoja juu ya hoja
 
Hoja juu ya hoja
saluni.jpg

Dawa za kulainisha nywele (relaxer) zimekuwa zinapendwa na wanawake wengi wa Afrika kwa kuwa zina uwezo wa kulainisha nywele na kumfanya apendeze na awe wa kuvutia.

Tatizo ni hili kusababisha uvimbe kwenye mji wa mimba, kwa nini wasiache na wabaki na nywele za kawaida ambazo haziwaletei madhara? Vinginevyo wanajitengenezea maafa kwa kujua na kutaka.
 
Tatizo ni hili kusababisha uvimbe kwenye mji wa mimba, kwa nini wasiache na wabaki na nywele za kawaida ambazo haziwaletei madhara? Vinginevyo wanajitengenezea maafa kwa kujua na kutaka.
Hawawezi kukuelewa tena ukipinga sana unaweza sababisha mtafaruku hapa, halafu wanakuwa na nywele nzuri sana sasa sijui kwanini wanaenda kujiharibu na madawa kichwani, wengine wanaenda kubandika yale manywele rangi ya kamba ya mkonge
 

Nimekuelewa sana muandishi, whether its a song, poem or whatever, I found myself somewhere inside there.......emotions
 
Back
Top Bottom