Tiba
JF-Expert Member
- Jul 15, 2008
- 4,604
- 3,163
Jana usiku nilipata taarifa kutoka kwa jamaa yangu mmoja anayeishi Rome, Italy kwamba ndugu yake wa kike aliyekuwa amemwalika kumtembelea pale Roma, alizuiliwa uwanja wa ndege wa Fumicino yeye na wanawake wengine kama ishirini hivi kutoka mataifa mbali mbali ya kiafrika waliosafiri na ndege ya Ethiopia Airline kutoka Addis. Walizuiliwa uwanja wa ndege pamoja na kwamba walikuwa na entry visa bila maji wala chakula tangia saa 12.45 asubuhi ndege ilipofika mpaka saa 7.00 kamili usiku wa kuamkia leo walipondishwa ndege hiyo hiyo ya Ethiopia Airline kurudishwa makwao.
Mwezi karibu mmoja uliopita, huyu jamaa yangu aliniomba nimsaidie kushughulikia visa ya mdogo wake na alimtumia barua ya mwaliko pamoja na tiketi ya kwenda Rome na kurudi huku akiambatanisha bank statement. Tulipowasilisha documents pale ubalozi wa Italy Upanga, maombi yalikubaliwa na Ijumaa ya tarehe 11/06/2010 tuliitwa kwenda kuchukua visa. Huyu dada aliondoka Dar jioni ya Jumapili ya 13/6/2010 na kufika Roma, Italy saa 12:45 asubuhi jana 14/6/2010.
Baada ya kuzuiliwa, hawakuruhusiwa kuwasiliana na ndugu zao na huyu jamaa yangu alinipigia simu kuniuliza kama kweli mdogo wake alipanda ndege pale Dar. Nilimuhakikishia kwamba aliondoka Dar. Hiyo ilikuwa ni baada ya kusubiri masaa 3 pale uwanjani bila mdogo wake kutokea. Niliwasiliana na Ethiopia airline kuangalia kama labda aliachwa pale Addis lakini walinitaarifu kwamba aliondoka Addis kueleka Roma. Saa nane mchana ndio walimruhusu kuwasiliana na kaka yake na kumweleza kuwa wamemzuilia kwa kuwa alisahau kuja na copy ya barua ya mwaliko. Kaka aliomba namba ya fax ili awatumie hiyo barua ya mwaliko kitu ambacho kilifanyika na fax kutumwa. Mpaka saa 11.00 jioni wakawa bado hawajamruhusu kutoka pamoja na kutumiwa barua ya mwaliko waliyokuwa wanaitaka. Ilibidi kaka mtu arudi tena airport akiwa na vitihibitsho vyote kuonyesha kwamba yule ni mgeni wake halali. Hakuna aliyekubali kumsikiliza kwa maelezo kwamba mwenye uwezo wa kutoa maamuzi hakuwepo kwa wakati huo labda mpaka kesho. Jamaa ilibidi arudi nyumbani ili kusubiri hiyo kesho. Cha ajabu alipigiwa simu na mdogo wake kwenye saa saba usiku wa kuamkia leo kwamba wanapandishwa kwenye ndege kurudishwa nyumbani yeye na waafrika wengine waliokuwa wamezuiliwa. Hivi ninavyoandika, muda is mrefu atakuwa anatua Dar Es Salaam.
Kuna masuala kadhaa hapa ya kujiuliza;
1. Je ni halali kumzuilia mtu kuingia kwenye nchi pamoja na kuwa na valid entry visa?
2. Kwa nini ubalozi wa Italy ulitoa visa kama walijua kwamba policy ya serikali yao kwa sasa ni kuzuia wanawake weusi kuingia Italy? Kwangu solution rahisi ingekuwa kumyima mtu visa kuliko kumzuilia kuingia wakati tayari ameingia gharama za usafiri!!!
3. Je ni sahihi kwa nchi inayosemekana ni ya ulimwengu wa kwanza kuwafanyia watu ubaguzi wa namna hii?
Tujadili.